in

Jinsi ya Kujua ni Laptop Gani ya Kununua Mwaka 2018

Hizi hapa ndio njia za kufuata wakati wa kununua laptop

laptop

Ni laptop gani ya kununua ni swali ambalo huulizwa sana na watu wengi lakini inapokuja katika swala la kununua computer ni vyema ukajua ni kitu gani unachotafuta katika computer na ni kiasi gani cha pesa uko tayari kutumia kununua laptop hiyo.

Kwa mfano kama wewe unataka kuwa na laptop ya kufanyia kazi ni vizuri ukatafuta laptop ambayo ina uwezo mkubwa kidogo tofauti na mtu ambaye anatafuta computer kwaajili ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii, pia swala la bajeti ni muhimu sana kama unatafuta laptop ya kuingia kwenye mitandao ni vyema ukaweka bajeti ndogo ya kawaida tofauti na yule anaetafuta laptop kwaajili ya kazi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Lakini pia katika kununua laptop kuna mambo kadhaa ya msingi ya kuzingatia iwe unataka laptop kwaajili ya kazi au kwaajili ya matumizi ya kwako ya kawaida ni vyema kuyajua mambo haya ili uweze kupata laptop ambayo ni bora kwa matumizi yako ya mwaka 2016, kama unavyojua laptop computers ni nyingi sana kwa sasa hivi hivyo inakuwa ni ngumu sana kuchagua ni laptop ipi itakayo kufaa wewe na matumizi yako hivyo basi yafuatayo ni mambo ya muhimu ambayo yataweza kukusaidi kujua ni computer ipi bora inayoweza kukufaa kwa matumizi ya mwaka 2016.

Kitu cha kwanza cha kuangalia katika kununua laptop ni “PROCESSOR” ni vyema kuangalia sana hii wakati unanunua computer yako, kwa kawaida laptop nyingi za sasa zinatumia Processor za Intel na ndio processor ambayo mimi ningependa kukushauri uchague kwenye laptop yako ijapokua kuna processor nyingine nyingi zenye nguvu kama AMD na nyingine nyingi ila ni vyema ukachagua processor ya Intel ambazo ni Intel Core i3, Intel Core i5 na Intel Core i7 ni vizuri pia ukaachana na processor za Intel Pentium na Intel Atom kwani hizi huwa na uwezo mdogo sana.

Kitu cha pili ni RAM au memory hii pia ni sehemu nyingine muhimu sana ya kuangalia wakati wa kutafuta laptop yako, kama laptop unayotaka kununua ni 32bit laptop hiyo itakuwa na uwezo wa kuongezea ram mpaka GB 3 tu na kama laptop unayotaka kununua ni 64bit laptop hiyo itaweza kuongezewa ram kwa kiasi kikubwa utakacho taka kuliko computer zile za 32bit, kwa hiyo ni vyema kukumbuka kuwa ukubwa wa ram unafanya computer yako kuwa haraka zaidi hivyo basi ni vyema kununua laptop yenye uwezo wa 64bit ili kupata laptop ambayo itakuwa na ubora zaidi na inayofanya kazi haraka.

Kitu cha tatu ni STORAGE hili ni tatizo kubwa sana linalowafanya watu wengi kuwa na wasi wasi wakati wa kununua laptop lakini hapa kuna siri ambayo watu wengi hawaijui, laptop nyingi za bei rahisi huja na hard disk ambazo huwa zinaitwa HDD au “Hard Disk Drive” ambazo hizi ndio zile ambazo zinakuwa zinazunguka kwa ndani pia HDD nyingi zinakuwa na nafasi kubwa lakini tatizo la HDD huwa hazidumi kwa muda mrefu hii inatuleta kwenye laptop za bei ghali, nyingi ya hizi laptop za bei ghali huja na hard disk zinazoitwa SSD au “Solid State Disk” ambazo mara nyingi hizi huja na nafasi ndogo kuliko zile za HDD lakini tofauti ya hizi ni kwamba SSD  hudumu kuliko zile za HDD na huwa zinasoma kwa haraka zaidi hivyo basi kama unaweza ni vyema ukanunua laptop zenye SSD Hard disk.

Kitu cha nne ni BATTERY kama unataka kununua laptop ni vyema ukaangalia battery yake inauwezo wa kukaana chaji muda gani na inaukubwa gani watu wengi kwa sasa huwa wananunua laptop kwa kuangalia muda wa chaji wa laptop, lakini  kama wewe unakuwa unafanyia kazi za kuwa unasafiri sana au sehemu ambazao hazina umeme ni vyema ukatafuta laptop yenye uwezo wa kukaa sana na chaji ila kama wewe utakua sehemu zenye umeme mara mara utakuwa huna wasi wasi wa kutafuta laptop inayokaa sana na chaji na pia utatumia kiwango kidogo cha pesa kuinunua.

Kitu cha tano ni SAIZI YA KIOO ni vyema kuangalia sizi ya kioo wakati wa kununua laptop kwani kwa sasa laptop zinatenenezwa zikiwa na vioo vya saizi mbalimbali hvyo basi kama laptop yako itakuwa inatumiaka sana ofisini au nyumbali ni vyema ukatafuta laptop yenye kioo kikubwa kidogo ila kama unatumia laptop yako safari ni vyema utafuta screen ndogo kidogo kwani itakuapa urahisi katika kuibeba pamoja na kuiifadhi. ila kumbuka sio kila kioo kimetengenezwa kwa teknolojia zinazo fanana mara nyingi laptop nyingi zenye vioo vikubwa sana hua hazina picha angavu ukilinganisha na zile zenye vioo vya saizi ya kawaida hivyo basi ni vizuri kuangalia hilo pia.

Kitu cha sita ni MUUNDO laptop sasa zipo zenye miundo tafauti tofauti hvyo ni vyema kuangalia muundo ambao ni bora ni vyema kuangalia Keyboard nzuri inayoeleweka, Mouse nzuri aliyoko fasta  na mengine mengi, hivyo basi ni vizuri kama utaweza kutumia laptop yako kabla hauja inunua ili kuweza kuangalia vitu hivi kwani laptop ikiwa na muundo bora basi uwezekano wa laptop hiyo kukaa kwa muda mrefu ni mkubwa.

Kitu cha saba na cha mwisho ni CONNECTIVITY au viunganishi ni vyema kuangali kwenye laptop hiyo kwamba inayo port ngapi za USB na kama inayo HDMI pia ni vyema kuangali kama inayo WIFI pamoja na BLUETOOTH kumbuka ni vyema kupata laptop yenye Speed ya WIFI  ya “802.11b/g/n 802.11ac” kama huna utalamu wa kuangali hii ni vyema kuangalia kwenye internet kwa ku-google jina la laptop na model yako.

Hivyo ndio vitu muhimu ambavyo ukiangalia kwenye laptop yako utakuwa umefanikiwa kupata laptop bora na nzuri kwa matumizi ya mwaka 2016, kwa wale wanao jiuliza kwanini sijaitaja Graphics hii ni kwa sababu laptop nyingi zinazokuja na processor ya Intel Core i3, Core i5 na Core i7 nyingi huja na Graphics ambayo ni nzuri sana hivyo huna haja ya kuwa na wasi wasi na hilo ila kama utanunua compute ya tofauti na hivyo ni vyema kuangalia kiwango cha Graphics kisiwe chini ya MB 1200.

Jinsi ya Kujua ni Laptop Gani ya Kununua Mwaka 2018
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Njia Bora ya Kudhibiti Matumizi ya Smartphone kwa Watoto

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

13 Comments

  1. Samahani jamani mimi nataka kunuwa laptop lakini yote hayo niliyo yasoma humondani bado baadhi sijayaelewa vizuri ndung na natafuta kwaajiri ya matumizi ya kazi pamoja na nyumbani , sasa sijuwi utani saidiaje sas ndugu

  2. Asante sana Joseph, ili kusudi upate laptop inayofaa nilazima wewe mwenyewe ujue ni laptop gani unayoitaji, ukishajua hilo ndipo utafute ushauri kwani kila mtu anamachaguzi yake pale inapokuja kwenye ununuzi wa vitu hasa vya electronics.
    Maana yangu ni kwamba inakubidi kuchagua kwanza aina ya laptop unayoitaji kwa kuangalia vigezo unavyoitaji kama vile RAM, HARD DISK au hata ukubwa wa laptop alafu baada ya hapo kabla ya kununua unaweza ukaomba ushauri kwa ndugu, rafiki au hata hapa tanzania tech hapo tutaweza kukushauri ni laptop gani ya kununua…..