Jinsi ya Kuangalia Kama Simu Yako ni Feki

Jinsi ya Kuangalia Kama Simu Yako ni Feki Jinsi ya Kuangalia Kama Simu Yako ni Feki

Kutokana na tangazo lililotolewa na mamlaka ya mawasiliano tanzania TCRA kwamba simu zote bandia zitafungiwa ifikapo mwezi june siku ya tarehe 16, watu wengi nchini tanzania wameanza kufanya hatua mbalimbali za kuangalia simu zao ili kujua kama ni feki.

Lakini njia iliyotangazwa na vyanzo mbalimbali ni njia ngumu sana, tena ukizingatia ni lazima uandike namba ya utambulisho yani IMEI pembeni ndipo utume meseji pia ni ngumu zaidi kwa watu wanaotumia simu za kugusa kioo yani smartphone kwani pale mwanga wa kioo unapozima wakati unaandika nilazima uanze tena zoezi hilo ili kuaandika namba hiyo ya utambulisho yani IMEI.

Advertisement

Ifuatayo ni njia rahisi kabisa ya kuangalia kama simu yako ni feki bila kupoteza muda kabisa, njia hii ni ya haraka sana na inafanya kazi kwenye kila mwenye smartphone Kama wewe unatumia smartphone yenye Play Store bofya hapo chini

Find IMEI
Price: Free

Utapelekwa moja kwa moja kwenye Play Store ya simu yako kisha pakua programu hiyo kwenye simu yako, pia kama simu yako haina Play Store pakua programu hiyo maalumu kwa Android Hapa

Ukisha pakua programu hiyo iwashe kisha utaona  IMEI ya simu yako baada ya hapo Bofya namba hiyo ya IMEI ili kuicopy kisha moja kwa moja nenda katika sehemu yako ya kuandika ujumbe mfupi kisha weka kidole kwa muda kama wa sekunde moja kisha bofya PASTE utaona namba yako ya IMEI kisha tuma namba hizo kwenda namba 15090.

Au unaweza kuingia kwenye website ya TCRA hapa TCRA.co.tz na PASTE IMEA ya simu yako hakikisha simu yako imeunganishwa na Internet. Bila shaka imekurahisishia kazi kidogo tuambie kama imekusaidia kwa kujifunza zaidi angalia video hapo juu.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use