Google Yapanga Kuondoa SMS Kwenye Android na Kuleta RCS

Google Yapanga Kuondoa SMS Kwenye Android na Kuleta RCS Google Yapanga Kuondoa SMS Kwenye Android na Kuleta RCS

SMS ni mfumo uliokwepo karibia miaka 30 iliyopita, SMS ni sehemu ya maisha ya watanzania wengi lakini kwa watu wengi watumiao smartphone SMS imeonekana kama ni mfumo usio wa ulazima sana ukitegemea hasa kuna application kama vile WhatsApp na nyingine nyingi.

Hivi karibuni Google imetangaza kuleta huduma mpya itakayo kuwepo kwa watu wote watumiao Android, huduma hiyo iitwayo “Rich Communications Services” au RCS ni huduma itakayo ondoa matumizi ya Whats App na SMS kabisa kwani ni bora kuwa na application moja itakayo fanya vitu vyote kwa pamoja kuliko kuwa na application inayofanya kazi moja. Application hiyo ya RCS itakuwa ikifanya kazi kama SMS na vilevile itakua ikifanya kazi kama Whatsapp maana yake ni kwamba sasa utakuwa na uwezo wa kutuma picha na sauti kwa mtu yoyote kwa kutumia RCS ambayo itakuja tayari kwenye simu yako kama vile SMS.

Application hiyo itatolewa na google hivi karibuni na itakuwa ikitokea kwenye kampuni iitwayo “JIBE” SOMA HAPA ZAIDI >>> JIBE

Advertisement

Watumiaji wote wa android wataweza kutumia application hiyo kama SMS, hivyo basi hivi karibun iitakuwa ukinunua simu yoyote smartphone hautatumia application ya SMS tena bali utatumia RCS.

Je unataka kujua lini application hiyo itatoka ?. Jiunge hapa ili kupata taarifa ya lini application hiyo inatoka JIUNGE HAPA NA GOOGLE

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use