Tamthilia ya Apple Planet of apps

Apple Yatarajia Kutoa Tamthilia Inayoitwa Planet of the Apps

Mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya Apple ilitangaza kuwa inafanya maandalizi ya script ya tamthilia yake mpya ambayo itakuwa ikijihusisha na watengenezaji wa programu mbalimbali au developers siku zimepita sasa kampuni hiyo leo ilitoa taarifa ya kuwa tamthilia hiyo imepatiwa jina. hata hivyo vyanzo vya habari katika blog mbalimbali za teknolojia za nchini marekani zinasema kuwa sasa tamthilia hiyo imepatiwa jina la Planet of the Apps.

Habari hizo zinaendelea kusema kuwa Apple imesha anza kukusanya waingizaji mbalimbali kwaajili ya tamthilia yake hiyo ambayo inategemewa kutoka mwishoni mwa mwaka huu, hata hivyo apple ilisema kwa sasa inatafuta watu 100 ambao wana ujuzi mkubwa wa utengenezaji wa programu mbalimbali ambao watakuwa wakishiriki katika tamthilia hiyo ambapo watakuwa na timu zao katika tamthilia hiyo mpya iliyopewa jina la Planet of the Apps.

Hata hivyo bado haijajulikana moja kwa moja kuwa tamthilia hiyo itakuwa ikionyesha nini bali watu mbalimbali duniani wanaonekana kudhani kuwa show hiyo itakuwa ikionyesha mashindano ya utengenezaji wa programu mbalimbali za kampuni hiyo kubwa nchini marekani.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii kwenye facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
NOte 7
Samsung Note 7 Ndio Simu ya Bei ya Ghali Kutoka Samsung
Next Post
Nokia P1

Nokia P1 Simu Mpya Kutoka Nokia Yenye Kutumia Android