Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WhatsApp Yaja na Username Badala ya Namba ya Simu

Sasa utaweza kutumia username na utaweza kuficha namba ya simu kwa watumiaji wapya
WhatsApp Yaja na Username Badala ya Namba ya Simu WhatsApp Yaja na Username Badala ya Namba ya Simu

WABetaInfo, chapisho linalojulikana kutoa taarifa za WhatsApp, lime gundua kipengele kipya katika toleo la hivi karibuni la WhatsApp beta toleo la Android 2.24.18.2.

Kwa wale ambao hawajui, WhatsApp tayari imeanza kufanya majaribio ya kipengele cha kuweka jina la mtumiaji (username), ambacho kiliripotiwa kuanza majaribio ya ndani kwenye toleo la WhatsApp beta kwa Android 2.23.11.15 mwezi Mei 2023.

Advertisement

Kipengele hiki kitawawezesha watumiaji kuchagua jina la mtumiaji au username jina ambalo mtumiaji anaweza kutumia badala ya namba ya simu. Ingawa kipengele hiki bado kipo kwenye hatua za majaribio kwenye WhatsApp beta ya Android, kampuni hiyo kubwa ya mitandao ya kijamii inaboresha zaidi kipengele hiki kwa kuongeza msaada wa PIN.

Sehemu hii ya username inaondoa hitaji la kushiriki namba yako ya simu na kuruhusu watu kuwasiliana na wewe kwenye WhatsApp kupitia username na kuzuia watu kuweza kuona namba yako ya simu moja kwa moja.

WhatsApp Yaja na Username Badala ya Namba ya Simu

Hata hivyo kupitia sehemu hiyo watu ambao tayari wana namba yako ya simu wataendelea kuiona, lakini unaweza kuchagua kutumia username pekee pale utakapo anzisha mazungumzo mapya au new chats.

Ili kuimarisha zaidi na kuongeza safu ya ziada ya faragha, WhatsApp pia ina tengeneza kipengele cha hiari cha PIN kwa ajili ya username, hasa kwa watu ambao unawasiliana nao kwa mara ya kwanza.

Kupitia username PIN, Mtumiaji anaweza kuweka PIN maalum kwenye username yake na pale mtu ambaye hajawahi kuwasiliana nae atakapo hitaji kutuma ujumbe ata lazimika kuweka PIN ya username ambayo ataipata kutoka kwa mtumiaji kabla ya kuwasiliana kupitia WhatsApp.

Kwa sasa sehemu hii inapatikana kwenye toleo la WhatsApp ya kawaida ya Majaribio maarufu kama WhatsApp Beta. Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa WhatsApp Beta jaribu sehemu hii. Kwa habari zaidi pakua app ya Tanzania Tech kupitia Play Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use