WhatsApp Yaongezewa Ulinzi Mpya wa Two-Step Verification

Kwa mara nyingine tena WhatsApp yaleta ulinzi mwingine tena wa Two-Step Verification
Two-Step Verification Two-Step Verification

Siku za karibuni WhatsApp imeonekana kuongeza ulizi zaidi kwenye programu zake za WhatsApp za Android na iOS. Hatua hizi zimekuja baada ya watu kuonekana kulalamika sana kuhusu kukosa ulinzi kamili kwenye programu hiyo maarufu ya kuchat, sababu hizo na nyingine nyingi ndio sababu ya programu hiyo ya WhatsApp kuongezewa ulinzi zaidi wa Two-Step Verification.

Two-Step Verification ni ulinzi mpya wa programu ya whatsapp ambapo hapa utaweza kulinda programu yako ili mtu asiweze kusajili namba yako kwenye simu nyingine, kwa kutumia sehemu hiyo utaweza kuingiza PIN namba ambazo zitakuwa nne na kila mara unapo jisajili kwenye kifaa kingine utalazimika kuingiza PIN hizo ambazo zitakuwezesha kuwasha programu yako kwenye kifaa kingine. Pale unapokuwa umesahau PIN yako utaweza kubadili PIN yako kwa kutumia Email ambayo utakuwa umeiweka mwanzoni utakapo wahsa sehemu hiyo.

Sehemu hiyo mpya kwa sasa inapatikana kwenye programu ya WhatsApp Beta kupitia sehemu ya Account Settings kisha Two-Step verifications hapo utaweza kuwasha au kuzima sehemu hiyo mpya ya ulinzi. Sehemu hii inategemewa kuja hivi karibuni hivyo kama umeona update za programu hiyo ni vizuri ukafanya update ili kujaribu sehemu hiyo. Kama unataka kujaribu sehemu hiyo mpya kwa sasa unaweza kujiunga na programu ya WhatsApp Beta kupiti Play Store.

Advertisement

Je unaonaje kuhusu maboresho haya kutoka WhatsApp..? tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use