Wapenzi wa Mpira wa Miguu na Simu za Tecno Mjiandae na Hii

Kampuni ya Tecno imeamua kuja na hii kwaajili ya mashabiki wa mpira
Tecno Camon CX Manchester City Edition Tecno Camon CX Manchester City Edition
Tecno Camon CX Manchester City Edition

Kampuni maarufu Africa kwa kutengeneza simu za mkononi yaani Tecno Mobile hivi karibuni imefanikisha kuingia makubaliano ya kibiashara na timu kubwa ya mpira wa miguu ya uingereza ya Manchester United ambapo kampuni hiyo imepanga kutoa simu zenye ubora huku zikiwa na rangi pamoja na nembo ya timu hiyo, imeripoti gazeti la nipashe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Kampuni hiyo itatumia uhusiano huo katika biashara hasa kwa wapenzi wa soka kwa kuleta bidhaa zenye ubora ambazo zitakuwa na alama ya timu hiyo maarufu na yenye wapenzi wengi nchini.

“Tolea maalum la simu hii awali ya yote itakua na alama ya timu ya Manchester City nyuma kwa chini ili kuleta ladha ya klabu hiyo mikononi mwa watumiaji.

Advertisement

Huku kioo cha simu hii kina ukubwa wan chi 5.5 FHD Inayotoa nafasi kwa mtumiaji kuangalia video vizuri kabisa, mteja wa Tecno Mobile akiishika simu hii sio tu kwamba itampa `ujasiri wa kuonyesha mbele za watu bali pia raha ya kuitumia,” ilisema Taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo inaeleza kuwa Tecno Camon CX yenye 16mp mbele ni toleo maalumu la klabu ya Manchester city na ni simu inayokwenda kwa wakati na yenye uwezo wa kupiga picha katika mwanga mdogo pia flashi mbili mbele zinazosaidia kupiga picha za mbele kuwa daraja la juu.

Muonekano wa mwisho wa simu hii unaonesha ni kwa jinsi gani simu hii inakuja na muonekano wa kibabe lakini ukiwa umebeba 64GB za kuhifadhi vitu ndani ya simu bila kutumia memori kadi ya nje huku ikipewa RAM ya 4GB inayotoa nafasi ya kutumia Zaidi.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Nipashe

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use