Vodacom na iFlix Zaungana Kuwezesha Wateja Kuangalia Filamu

Sasa utaweza kuangalia filamu kwa kutumia vifurushi maalum vya Vodacom
IFLIX na Vodacom IFLIX na Vodacom

Kampuni ya kutoa huduma za simu ya Vodacom Tanzania, hivi leo imetangaza kuingia ubia na kampuni ya iFlix kuwezesha wateja wake kuweza kuangalia filamu kwa haraka kwa kutumia mtandao wa 4G wa Vodacom.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano huo, mmoja wa wazungumzaji kutoka Vodacom alisema kuwa mtandao wa 4G wa Vodacom Tanzania hivi karibuni umeongezewa kasi na kuwa Super Network kitendo ambacho kina ruhusu mtu kuweza kuangalia video za live au mubashara bila kupata usumbufu wa kukata kata.

Mbali na hayo msemaji huyo alisema kuwa kupitia programu na mtandao wa iFlix wateja wataweza kutumia internet au vifurushi maalum vya bando ambavyo vitapatikana kupitia mtandao wa Vodacom ili kukuwezesha kuangalia filamu kupitia mtandao wa iFlix kwa haraka bila kukata kata. Hata hivyo msemaji huyo alisema kuwa, kwa muda huu wakati Vodacom ndio imetangaza ushirikiano huo na kampuni ya iFlix wateja wa mtandao wa Vodacom wataweza kuangalia filamu na Tamthilia kupitia programu hiyo bure kabisa mpaka hapo ifikapo mwezi ujao.

Advertisement

Kama ulikuwa uhifahamu iFlix, Huu ni mtandao kama Netflix ambao wenyewe pia unakuwa na filamu mbalimbali za nje na ndani ya Afrika pamoja na Tamthilia mbalimbali ikiwa pamoja na makala mbalimbali. Kama unatumia mtandao wa Vodacom na upo Tanzania unaweza kupakua programu ya iFlix kwa kutumia link hapo chini na kujaribu kama utaweza kuangalia filamu bure kama vodacom inavyosema.

  • iFlix – Android 
iflix: Asian & Local Dramas
Price: To be announced
  • iFlix – iOS

Kwa sasa tumesha wasiliana na Vodacom kwaajili ya kupata habari zaidi kuhusu hili hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi pale tutakapo pata taarifa zaidi kutoka Vodacom.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use