Vodacom Yabadili M-Pesa Mastercard Kwenda M-Pesa VISA Card

Vodacom Tanzania imetangaza mabadiliko hayo leo tarehe 30/10/2021
Vodacom Yabadili M-Pesa Mastercard Kwenda M-Pesa VISA Card Vodacom Yabadili M-Pesa Mastercard Kwenda M-Pesa VISA Card

Kampuni inayotoa huduma za simu ya Vodacom Tanzania, hivi leo imetangaza kuamia kwenye huduma za malipo ya mtandaoni ya M-Pesa Visa Card badala ya M-Pesa Mastercard iliyo kuwa inatumika awali.

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa huduma ya zamani ya M-Pesa Mastercard, inawezekana umepokea ujumbe mfupi ambao unakutaarifu kuwa huduma ya M-Pesa Mastercard haito kuwepo tena badala yake umeletewa huduma bora zaidi.

Vodacom Yabadili M-Pesa Mastercard Kwenda M-Pesa VISA Card

Advertisement

Kama wewe ni mmoja wa watu walio pokea ujumbe huu, moja kwa moja utakuwa umerudishiwa pesa zako zilizokwepo kwenye huduma hiyo ya M-Pesa Mastercard na sasa ni lazima kutengeneza kadi nyingine ya M-Pesa Visa ili kuendelea kupata huduma hii.

Hadi sasa bado hakuna taarifa kwanini Vodacom imefanya mabadiliko hayo, na bado hakuna taarifa kama mabadiliko haya ni ya kudumu au yamefanyika kwa muda mfupi.

Tofauti ya M-Pesa Mastercard na M-Pesa VISA Card

Ni wazi kuwa kwa mtumiaji kama wewe na mimi swali ambalo linakuja kwako ni, je kuna tofauti gani kati ya VISA na Mastercard.

Vodacom Yabadili M-Pesa Mastercard Kwenda M-Pesa VISA Card

Kama wewe ni mtumiaji wa huduma hii na unataka kujua tofauti ya M-Pesa Mastercard na M-pesa VISA basi moja kwa moja huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani M-Pesa Mastercard na M-Pesa VISA Card hazina tofauti sana japokuwa hizi ni kampuni mbili tofauti.

Kwa upande wa matumizi ya M-Pesa VISA Card, bado binafsi sijajua kama kuna faida au hasara ya kubadilisha kutoka Mastercard kwenda VISA. Kwani hadi sasa utaratibu wa kutengeneza kadi ni ule ule na bado unaweza kutumia kadi yako kufanya manunuzi mtandaoni kama ilivyokuwa kwenya M-Pesa Mastercard.

Kama unataka kujua tofauti ya Mastercard na VISA kwa undani zaidi basi unaweza kusoma zaidi hapa.

Jinsi ya Kutengeneza M-Pesa VISA Card

Kama unataka kufanya manunuzi mtandaoni au kulipia huduma mbalimbali mtandaoni unaweza kutengeneza M-pesa VISA Card kwa urahisi kwa kufuata hatua hizi rahisi.

Njia ya USSD Code

  1. Hatua ya kwanza bofya *150 *00 #
  2. Chagua namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
  3. Chagua namba 6 (M-Pesa VISA Card)
  4. Chagua namba 1 (Tengeneza Kadi)

Baada ya hapo utapokea namba za kadi yako zikiwa pamoja na CVV ambazo zipo idadi ya namba 3 na pia tarehe ya kuisha kwa muda wa kadi yako. Vitu vyote hivyo ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyo tumika kufanya malipo kwenye mitandao mbalimbali.

Kwa kufuata njia hiyo utakuwa uko tayari kuweza kufanya manunuzi mtandaoni kupitia M-Pesa VISA Card. Kwa habari zaidi kuhusu mabadiliko haya ya M-Pesa Mastercard kwenda M-Pesa VISA Card endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use