Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Baadhi ya mambo ya teknolojia yalioathiriwa na mlipuko wa virusi vya corona
Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020 Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Bado taarifa za virusi vya corona zinaendelea kuchukua vichwa vya habari mbalimbali duniani kote, na wakati vifo vikiendelea kuongezeka, ugonjwa huo umeonekana kuadhiri teknolojia kwa kiasi kikubwa sana.

Ikiwa ni takribani robo ya kwanza ya mwaka huu 2020, tayari kampuni mbalimbali za teknolojia duniani kote zimeonekana kufanya mabadiliko makubwa kutokana na ugonjwa huo, mabadiliko ambayo yanaweza kuadhiri teknolojia kwa kiasi kikubwa kwa mwaka huu 2020.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia baadhi ya mambo mbalimbali ya teknolojia ambayo kwa namna moja ama nyingine yamesababishwa na tatizo la ugonjwa huu wa corona na kusababisha kuadhiri utendaji wa makampuni mbalimbali ya teknolojia. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie mambo haya.

Advertisement

Kusitishwa Kwa Mkutano wa MWC 2020

Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Mkutano wa MWC au Mobile World Congress ni moja ya mkutano ambao unategemewa sana na makampuni mbalimbali ya teknolojia duniani. Mbali ya kutegemewa na makampuni ya kiteknolojia pia mkutano huo ni chanzo kikubwa sana cha ajira kubwa kwa watu mbalimbali ambayo hufanya kazi kwenye mkutano huo kila mwaka. Kuahirishwa kwa mkutano huo mwaka huu, kumesababisha baadhi ya kampuni kutozindua bidhaa zake ambazo mara nyingi zimekuwa zikizinduliwa kwenye mkutano huo.

Google na Facebook Zimesitishwa Mikutano Muhimu

Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Kampuni maarufu za teknolojia duniani za Google pamoja na Facebook, hivi karibuni zimetangaza kusitisha mikutano yao muhimu ambayo imekuwa ikitegemewa sana na kampuni hizo kuonyesha baadhi ya bidhaa zao mpya zinazokuja kwa mwaka huo.

Kwa mujibu wa tovuti ya taarifa ya Facebook, Facebook imetangaza kusitisha mkutano wake mkubwa wa F8 2020, mkutano ambao unalenga kuonyesha yale ambayo facebook inategemea kuyafanya kwenye huduma zake mbalimbali za mitandao ya kijamii pamoja na huduma nyingine zinazo milikiwa na kampuni hizo.

Apple Imetangaza Kutegemea Kupata Hasara Mwaka Huu

Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, kampuni ya Apple hivi karibuni ilitoa taarifa ya kuwa inategemea kutofikisha malengo yake ya mapato kwa mwaka huu 2020 kutoka na ugonjwa wa corona. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Apple imedai kuwa, kutokana na asilimia kubwa ya utengenezaji wa simu zake za iPhone na bidhaa nyingine kufanyika nchini China. Kampuni hiyo inategemea kuchelewa kukamilisha utengenezaji wa bidhaa hizo ikiwa pamoja na kufikisha bidhaa hizo kwa watumiaji kwa wakati kama ilivyo tarajiwa.

Facebook Yasitisha Kupokea Wageni Kwenye Ofisi Zake

Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo wa corona, hivi karibuni Facebook imetengaza kusitisha kupokea wageni kwenye ofisi zake huku ikiwahitaji wale wanaotegemea kupata ajira kwenye kampuni hiyo kufanya Interview kupitia mfumo wa Video.

Twitter Yatangaza Kusitisha Safari za Wafanyakazi Wake

Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Hivi karibuni Twitter ilitangaza kusitisha kusafiri kwa wafanyikazi wake ikiwa pamoja na safari ya kuelekea kwenye mkutano wake wa kila mwaka wa (SXSW), pamoja na safari zote kwajili ya matamasha na mikutano mbalimbali kutokana na wasiwasi juu ya kuenea kwa coronavirus.

Kampuni hiyo ilitangaza Jumapili kuwa imesimamisha kusafiri kwa biashara na hafla zote kabisa na itandelea kufanya hivyo hadi chanjo itakapopatikana, au hadi “Shirika la Afya Ulimwenguni au Vituo vya Udhibiti wa Magonjwa ya mlipuko (CDC) itakapo tangaza rasmi njia za kujikinga.

Mkutano Mkubwa wa Kuonyesha Magari Wasitishwa

Jinsi Virusi vya Corona Vinavyo Athiri Teknolojia Mwaka 2020

Mkutano wa Geneva Motor Show ambao hufanyika kila mwaka, hivi karibuni imutengazwa kusitishwa baada ya serikali ya Uswizi kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya elfu moja au zaidi kuanzia siku ya Ijumaa kutokana na wasiwasi juu ya kusambaa kwa virusi vya corona. Marufuku hiyo inafanya kazi mara moja na itaendelea angalau hadi Machi 15. Mkutano huo ulikuwa unatehemewa kuanza wiki ijayo.

Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanaendelea kwenye ulimwengu wa teknolojia ambayo yamekwama kutoka na kuendelea kwa virusi vya corona. Kwa sasa bado nchi mbalimbali zinaendelea kupambana na ugonjwa huo huku hadi sasa ikisemekana vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa huo vikifikia watu 3,164 kwa mujibu wa mtandao wa worldometers.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use