Vifurushi vya Bei Nafuu Kutoka Mitandao Mbalimbali ya Simu

Vifurushi vya muda wa maongezi, Internet pamoja na SMS
Vifurushi vya bei nafuu Vifurushi vya bei nafuu

Ukweli ni kwamba ni watu wachache sana siku hizi hupiga simu na kutumia Internet pamoja na kutuma SMS kwa kutumia salio la kawaida, yote hiyo ni sababu ya ujio wa vifurushi ambavyo watu wengi hutumia ili kubana matumizi na kuepukana na gharama zisizokuwa na ulazima.

Lakini kadri siku zinavyo zidi kwenda gharama za vifurushi hivi zinazidi kupanda kwa kasi na hii kusababisha matumizi ya simu kuwa magumu na kupelekea wateja wa mitandao kuhama hama kila mara. Sasa kuliona hilo leo Tanzania Tech tumekuletea aina mbalimbali za vifurushi vya bei nafuu ikiwa pamoja na njia za kuweza kujiunga na vifurushi hivyo.

Vifurushi hivyo vimejipanga kulingana na mtandao hivyo hakikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu kila siku kwani tutakuwa tukiweka aina mpya za vifurushi pindi tutakapo kuwa tumevipata, basi bila kupoteza wakati basi twende tukangalie vifurushi hivi.

Advertisement

Vodacom Tanzania

Kama wewe upo Dar es salaam basi unaweza kufaidi kifurushi cha DAR SUPA UNI kwani kifurushi hichi ni cha gharama nafuu sana. Kifurushi hichi kinakupa.

MUDA – Masaa 24 (Kwa Siku)

 • Voda kwenda Voda – Dakika 30
 • Mitandao Yote – Dakika 20
 • SMS – 500
 • Internet – MB500
 • Bei – Tsh 500

MUDA – Masaa 24 (Kwa Siku)

 • Mitandao Yote – Dakika 55
 • SMS – 50
 • Internet – Haina Internet
 • Bei – Tsh 1000

MUDA – Siku 7

 • Voda kwenda Voda – Dakika 150
 • Mitandao Yote – Dakika 50
 • SMS – 2000
 • Internet – GB 1
 • Bei – Tsh 2000

Vifurushi hivi vingi vinakuja na WhatsApp, Facebook na Instagram bure kabisa kwa muda ambao kifurushi chako kitakuwepo, yaani kama ulinunua kifurushi cha Masaa 24 WhatsApp, Facebook na Instagram zitakuwa bure kwa muda huo hata kama Dakika na MB zako zimekusha. Kama uko Dar es salaam unaweza kupata kifurushi hichi kwa kubofya *149*03#

Tigo Tanzania

Kwa upande wa Tigo vifurushi vingi vilivyopo ni vilevile vinavyopatikana kwenye menu ya kawaida ya *147*00# lakini pia kama unataka vifurushi vya muda wa maongezi unaweza kufuata hatua zifuatazo.

 • Andika SAA kupitia ukurasa wako wa SMS, Kisha tuma neno hilo kwenda namba 15509 kwa kufanya hatua hizi utaweza kupata muda wa lisaa limoja kuongea kwa gharama ya Tsh 100. Baada ya muda huu kuisha muda huo utaisha na ukiangalia kwa siku utakuta umetumia Tsh 2400.
 • Vilevile unaweza kupata vifurushi vingine kwa kupiga namba *148*03# au 148*02#

TTCL Tanzania

Kwa upande wa mtandao wa simu wa TTCL unaweza kupata bando la bei nafuu kwa kupitia menu ya *148*30# kisha chagua bandika bandua hapo utapata vifurushi vya internet nafuu zaidi. Unaweza kupata kuanzia MB 700 kwa siku kwa Tsh 500 na pia unaweza kupata hadi GB 8 kwa Tsh 5000, GB 3 utazitumia mchana hadi saa mbili usiku na GB 5 utazitumia kuanzia saa mbili usiku hadi saa 12 Asubuhi.

Halotel Tanzania

Kwa upande wa Halotel vifurushi vya bei nafuu zaidi vipo kwenye menu ya Vifurushi vya chuo ambavyo hivi ni lazima kupata laini ya Chuo. Unaweza kupata laini hii kwa mawakala wanaopita barabarani na hakikisha laini yako ni ya Chuo kabla ya kumpa hela. Ukishapata laini utapiga namba *148*55# alafu utaweza kupata vifurushi vya bei nafuu vya muda wa maongezi, SMS pamoja na Internet.

Airtel Tanzania

Kwa upande wa Airtel Tanzania unaweza kupata vifurushi vya bei nafuu kwa kubofya menu ya *149*99*03# na utapata vifurushi vya muda wa maongezi vya bei rahisi. Vilevile unaweza kupata vifurushi vya bei nafuu vya internet na muda wa maongezi pamoja na SMS kwa kubofya menu ya *149*99# kisha utaweza kuchagua UNI Ofa na hapo unaweza kupata vifurushi vya hadi kuanzia Tsh 500.

MUDA – Masaa 24 (Kwa Siku)

 • Airtel kwenda Airtel – Dakika 50
 • Mitandao Yote – Dakika 10
 • SMS – 1000
 • Internet – MB500
 • Bei – Tsh 500

MUDA – Kwa Siku 3

 • Airtel kwenda Airtel – Dakika 100
 • Mitandao Yote – Dakika 10
 • SMS – 1000
 • Internet – GB 1
 • Bei – Tsh 1000

MUDA – Siku 7

 • Airtel kwenda Airtel – Dakika 145
 • Mitandao Yote – Dakika 5
 • SMS – 1000
 • Internet – MB 750
 • Bei – Tsh 1500

Na hivyo ndio baadhi tu ya vifurushi ambavyo unaweza kupata kwa bei nafuu, kama kuna vifurushi vingine unavyo vijua unaweza kuhabarisha wengine kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech.

5 comments
 1. Kuna ile huduma ipo kwenye tigo ya kuandika neno bure namba nimeisahau ile huduma huwa inapatikana je wakuu?

 2. NINGEPENDA KUJIUNGA NA AIRTEL ILA NAJIULIZA JE VIFURUSHI VYAO HAVIBADILIKI MAANA KUNAMTANDAO NILIKUWA NATUMIA ILA VIFURISHI VYO VINABADILIKA KILA SIKU

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use