TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hii hapa list ya TV za Hisense ambazo unaweza kununua hapa Tanzania
TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023) TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta TV nzuri ya kununua ni wazi kuwa tayari umeshakutana na aina nyingi za TV, kupitia makala hii nitaenda kuonyesha TV nzuri za Hisense ambazo unaweza kununua kwa sasa.

Haijalishi upo sehemu gani kwa hapa Tanzania na uhakika utaweza kupata TV hizi moja kwa moja, basi bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende tuka angalie TV nzuri za Hisense ambazo unaweza kununua kwa sasa.

Kitu cha muhimu kumbuka kuwa zipo TV za aina mbili, yaani Smart TV ambazo hizi huwa na mfumo wa uendeshaji kama Android au Veeda Os. Pia zipo TV za kawaida ambazo hizi ni LED TV. Basi baada ya kuelewa hayo moja kwa moja twende tukangalie list hii.

Advertisement

Hisense LED inch 32

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense LED ya inch 32 ni TV nzuri ambayo unaweza kununua kwa sasa, TV hii inakuja na teknolojia ya LED na pia ina uwezo wa kuonyesha channel za ndani bure bila kuwa na kisibusi. TV hii inapatikana hapa Tanzania kwa bei ya makadirio kati ya TZS 450,000 – TZS 430,000.

Hisense LED inch 40

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense LED ya inch 40 ni moja kati ya TV nzuri ya kununua kwa sasa, TV hii inapatikana kwa bei nafuu na pia unaweza kuangalia TV za ndani bila kuwa na kisimbusi. TV hii inapatikana hapa Tanzania kwa bei ya makadirio kati ya TZS 630,000 – TZS 600,000.

Hisense LED Inch 43

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense LED ya inch 43 ni moja ya TV ambayo kwa sasa inapatikana sehemu nyingi, TV hii kama zilivyo TV zilizopita utaweza kuangalia channel za ndani kupitia TV hii bila kuwa na kisimbusi, pia utaweza kuangalia Movie mbalimbali kupitia flash pamoja na mambo mengine mengi. TV hii inapatikana hapa Tanzania kwa bei ya makadirio kati ya TZS 780,000 – TZS 750,000.

Hisense LED inch 49

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense ya inch 49 ni TV ni nyingine nzuri ambayo unaweza kununua kwa sasa, TV hii kama ilivyo ya inch 43 imetengenezwa kwa teknolojia ya LED na pia inakuja na uwezao wa kuonyesha channel za ndani bure bila kisimbusi. Pia inaweza unaweza kusikiliza Radio mbalimbali pamoja na kuangalia Movie kupitia sehemu ya Flash pamoja na kutumia HDMI. TV hii inapatikana kwa bei ya makadirio kati ya TZS 900,000 – TZS 880,000.

Hisense Smart TV inch 32

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense Smart TV ya inch 32 ni TV nyingine nzuri ya kununua kwa sasa, TV hii inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Veeda Os ambao unasaidia kupata programu mbalimbali kama YouTube, Netflix na progamu nyingine moja kwa moja kwenye TV yako. Pia unaweza kuunganisha na Internet TV hii moja kwa moja. Hisense Smart TV ya Inch 32 inapatikana kati ya TZS 530,000 – 500,000.

Hisense Smart TV Inch 43

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense Smart TV ya inch 43 pia ni TV nyingine nzuri ambayo unaweza kununua kwa sasa. TV hii inapatikana ikiwa na sifa mbalimbali kama vile uwezo wa kupakia apps mbalimbali, mfumo wa Veeda OS pamoja na sifa nyingine zote zinazopatikana kwenye TV zilizo tangakulia kwenye list hii. Unaweza kupata TV hii ya Hisense Smart TV ya inch 43 kwa bei kuanzia TZS 850,000 – TZS 800,000. Pia unaweza kupata TV ya Hisense Smart TV yenye OS ya Android kwa ongezeko la kati ya TZS 60,000 had 50,000 kwa bei husika hapo juu.

Hisense Smart TV inch 49

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense Smart TV ya inch 49 pia ni TV nyingine nzuri ambayo unaweza kununua kwa sasa, TV hii inapatikana kwa hapa nchini Tanzania ikiwa na uwezo wa kuonyesha channel za ndani bila kisimbusi, pia utaweza kuangalia movie na video kupitia sehemu ya Flash pamoja na uwezo wa kuhifadhi programu mbalimbali kupitia mfumo wake wa Veeda OS. Pia utapata sehemu za HDMI pamoja na optical kwaajili ya sauti. TV ya Hisense Smart TV ya inch 49 inapatikana kwa kati ya TZS 1,000,000 na TZS 950,000.

Hisense Smart UHD / 4K inch 43

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Hisense Smart TV yenye UHD 4K ya inch 43 ni TV nzuri sana ambayo unaweza kununua kwa sasa, TV hii inakuja na teknolojia bora zaidi kuliko TV zilizo tangulia kwenye list hii. Hiyo ni kutokana na uwezo wake wa teknolojia ya UHD 4K pamoja na sifa nyingine mbalimbali kama vile kisimbusi cha ndani kwaajili ya kuona channel za ndani, uwezo wa kupakia programu nyingi zaidi pamoja na sifa nyingine zote ambazo zipo kwenye TV zilizopita kwenye list hii. Hisense Smart UHD / 4K inch 43 inapatikana kwa bei kati ya TZS 930,000 – 850,000.

Hisense Smart UHD / 4K inch 50

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Kwa upande wa Hisense Smart UHD / 4K ya inch 50 pia TV hii inafanana na TV hapo juu utofauti mkubwa ukiwa ni ukubwa wa kioo. Kila kitu ambacho TV hapo juu inafanya basi pia TV hii ya Hisense Smart UHD / 4K inch 50 ina uwezo wa kufanya. TV hii inapatikana kwa hapa Tanzania kwa bei ya makadirio kati ya TZS 1,150,000 – TZS 1,100,000. Kwa TV ya aina hii yenye Android utaipata kwa Kati ya TZS 1,250,000 hadi TZS 1,200,000.

Hisense Smart UHD / 4K inch 55

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

TV nyingine nzuri ya kununua kutoka Hisense ni Hisense Smart UHD / 4K ya inch 55, TV hii inapatikana ikiwa na matoleo mawili tofauti, toleo ambalo linakuja na mfumo wa Android na toleo ambalo linakuja na mfumo wa Vidaa OS. TV zote za aina hii zenye mfumo wa Android au Vidaa Os zote zinakuja na sifa sawa kama vile teknolojia ya UHD / 4K, pamoja na uwezo wa kunyesha channel za ndan pamoja na uwezo wa kupakia programu mbalimbali.

Pia utaweza kuangalia video kupitia USB, pamoja na sehemu nyingi zaidi za HDMI. TV hii kwa sasa inapatikana kwa kati ya TZS 1,300,000 – 1,250,000 kwa TV yenye Vidaa OS, na kwa TV hii yenye Android inapatikana kwa kati ya TZS 1,400,000 – TZS 1,350,000.

TV Nyingine za Hisense na Bei Zake

TV Nzuri za Hisense Unazoweza Kununua kwa Sasa (2023)

Kumbuka kuanzia TV za inch 55 kuendelea bei inaweza kuwa kubwa zaidi kulingana na aina ya teknolojia za TV hizo. Kwa mfano TV ya Hisense yenye Model Number 558000UW inaweza kupatakana kwa bei ghali zaidi kuliko TV nilizotaja hapo juu. Unaweza kuona utofauti wa bei kwa kuangalia List hapo chini.

Kufahamu zaidi kuhusu TV hizi unaweza kubofya link kwenye sehemu ya Model na utapelekwa kwenye tovuti maalum ya Hisense ambapo unaweza kusoma sifa kamili za TV hizi.

Na hizo ndio TV nzuri za Hisense ambazo unaweza kununua kwa sasa, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kununua TV. Kama unatak kujifunza kwa vitendo hakikisha unatembelea channel yetu ya YouTube Hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use