TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Tecno Spark 7 Mwezi Huu

Tecno Spark 7 inatarajiwa kupatikana kwanza nchini India
TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Tecno Spark 7 Mwezi Huu TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Tecno Spark 7 Mwezi Huu

Kampuni ya TECNO hivi karibuni inategemea kuzindua simu mpya ya Tecno Spark 7 huko nchini India, simu hii inategemewa kufuata nyayo za Tecno Spark 6 ambayo haiku zinduliwa kwa hapa Tanzania.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, simu hiyo mpya inatarajiwa kuzinduliwa huko nchini India wiki hii siku ya tarehe 9 mwezi huu, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali tayari kampuni ya TECNO imesha tangaza kuwa simu hiyo itakuwa inapatikana moja kwa moja kupitia tovuti ya Amazon ya nchini India.

Kwa mujibu wa ukurasa ambao tayari upo kwenye tovuti hiyo ya Amazon, Tecno Spark 7 inatarajiwa kuja na battery kubwa ya 6000 mAh huku ikidaiwa kuwa simu hiyo inauwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa siku 41 ikiwa imewashwa na kama haito tumika yaani (Standby Mode).

Advertisement

TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Tecno Spark 7 Mwezi Huu

Kwa mujibu wa ukurasa huo, Tecno Spark 7 inatarajiwa kuja na kamera mbili kwa nyuma huku kamera ya mbele ikitarajiwa kusaidiwa na flash mbili ambazo zimejificha kwenye simu hiyo kwa juu kwenye upande wa kushoto na kulia.

TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Tecno Spark 7 Mwezi Huu

Mbali na hayo simu hii inatarajiwa kuja na mfumo mpya wa Android 11, huku ikiwa pia na toleo jipya la mfumo wa HiOS. Kwa sasa bado hakuna taarifa kama simu hii itakuja hapa Tanzania au kama itakuja ikiwa na jina lingine. Kufahamu hayo na mengine mengi endelea kutembelea Tanzania tech tutakujuza pindi tu tutakapo pata taarifa zaidi.

Pia kama unataka kujua zaidi kuhusu sifa na bei ya simu zote mpya zinazotoka mwaka huu unaweza kutembelea ukurasa wetu wa simu mpya hapa. Kwa taarifa zaidi na maujanja zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use