Jiandae na TECNO CAMON 18 Yenye Gimbal Kamera

Camon 18 ndiyo simu ya kwanza ya TECNO kuwa na Gimbal Camera
Jiandae na TECNO CAMON 18 Yenye Gimbal Kamera Jiandae na TECNO CAMON 18 Yenye Gimbal Kamera

Kuelekea mwisho wa mwaka 2021 kampuni ya simu za mkononi TECNO yenye mashabiki wengi hasa upande wa simu janja inatarajiwa kuzindua toleo jipya la mfululizo wa simu zake aina ya TECNO Camon 18 yenye ubora ulioboreshwa hasa upande wa picha na video.

Series ya CAMON imekuwa ikiaminika kuwa na simu zenye kamera kali kutoka kwenye kampuni hiyo, japo simu hiyo haijatambulishwa rasmi lakini tayari kuna tetesi huenda simu hiyo ni TECNO Camon 18.

Jiandae na TECNO CAMON 18 Yenye Gimbal Kamera

Advertisement

TECNO Camon 18 inasemekana kuja kuwa suluhisho kwa wenye uhitaji mkubwa wa kamera katika kazi za kila siku hata kwa waandishi wa habari itawasaidia katika kuchukua matukio kadha wa kadha ambapo ina Mega Pixel 64.

Simu hii inayosemekana kuwa camon 18 ndiyo simu ya kwanza TECNO kuwa na GIMBAL CAMERA hii ni kamera ya hali ya juu sana katika mfumo mzima wa uchukuaji video kuwahi kutokea TECNO ambapo inaweza kurekodi video HD katika mazingira yoyote yale hata kama mchukuaji video anakimbia au kutembea lakini video haitotingishika.

Jiandae na TECNO CAMON 18 Yenye Gimbal Kamera

Mfumo wa ufanyaji kazi wa Gimbal camera

Pia simu hii ya CAMON 18 ina kamera yenye uwezo mkubwa wa ku-zoom mara 60X Zaidi na kufanya kitu kilichokuwa mbali na kuwa karibu Zaidi. Bila kusahau main kamera ya CAMON 18 ina mega pixels zipatazo 64 za kukuwezesha kupiga picha safi katika mazingira ya usiku na mchana.

Jiandae na TECNO CAMON 18 Yenye Gimbal Kamera

Mfumo wa camera unavyozoom mara 60x zaidi

Pia wameboresha  uwezo wa kuhifadhia kumbukumbu  ni mkubwa zaidi ambapo itakuwa na  256GB ROM kwa 8GB RAM hivyo kuzidi kumvutia mteja kumiliki simu hii yenye uwezo mkubwa zaidi. Kufahamu Zaidi kuhusiana na CAMON 18 tembelea: shorturl.at/isvzM

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use