Jinsi ya Kugundua Mapema Tatizo Lolote la Simu Yako

Fahamu kwa haraka matatizo ya Simu yako ya Android au iPhone (iOS)
Jinsi ya Kugundua Mapema Tatizo Lolote la Simu Yako Jinsi ya Kugundua Mapema Tatizo Lolote la Simu Yako

Ukweli ni kwamba kila kifaa cha kieletroniki huonyesha dalili kabla ya kuharibika kwake, lakini watu wengi wamekuwa wakipuuza dalili hizo na hatimaye kifaa kuharibika bila kujua kuwa kifaa hicho kilishawahi kuonyesha dalili ya kuharibika.

Kuliona hili leo nimekuletea makala hii ambayo itakusaidia kugundua mapema matatizo mbalimbali ya simu yako ya Android au iOS kwa urahisi na haraka, basi bila kupoteza muda twende nikuonyeshe njia hii rahisi ambayo na hakika itakusaidia sana kugundua tatizo la simu yako.

Kwa Simu za Samsung

Kupitia simu za Samsung unaweza kupata Menu ambayo itakusaidia kufanya majaribio ya vitu mbalimbali kwenye simu yako.

Advertisement

Jinsi ya Kugundua Mapema Tatizo Lolote la Simu Yako

Majaribio hayo ni kama vile kujaribu spika za simu yako, mic, kioo, sensor za simu yako na vitu vingine vingi. Hakikisha unatumia menu hii kuweza kufanya majaribio haya angalau mara moja kwa mwezi, unaweza kupata menu hiyo kwa kubofya ( *#0*# ) Alama ya nyota + reli + sifuri + alama ya nyota + alama ya reli.

Kwa Simu Nyingine Zote za Android

Kama unatumia simu yoyote ya Android, hata kama ni Samsung unaweza kugundua matatizo mbalimbali kwa kufanya majaribio zaidi kuhakikisha kama simu yako inafanyakazi inavyostahili kwa kutumia njia hii rahisi.

Jinsi ya Kugundua Mapema Tatizo Lolote la Simu Yako

Kupitia soko la Play Store, pakua app inayoitwa TestM unaweza kupata app hii kupitia link hapa au unaweza kupakua kupitia hapo chini. App hii inakupa uwezo wa kufanya majaribio ya vitu mbalimbali kwenye simu yako ili kuhakikisha vinafanyakazi kwa asilimia 100. App hii ina uwezo mkubwa sana wa kufanya majaribio kwenye simu zote bila kujali aina ya simu unayotumia.

TestM
Price: Free

Kwa Simu za iPhone (iOS)

Kama unatumia simu ya iPhone basi pia unaweza kugundua matatizo ya simu yako mapema kwa kutumia njia hii rahisi na haraka.

Jinsi ya Kugundua Mapema Tatizo Lolote la Simu Yako

Kupitia soko la App Store, unaweza kudownload app ya Phone Diagnostics, app hii itaweza kusaidia sana kugundua matatizo ya simu yako ya iPhone au hata iPad. Kama unaona simu yako haifanyi kazi vizuri basi unaweza kuinstall app hiyo na kufanya majaribio ili kugundua tatizo la simu yako.

‎Phone Diagnostics
Price: Free+

Njia Nyingine

Kama kwa namna yoyote njia moja kati ya hizo hapo juu haifanyikazi kwenye simu yako basi unaweza kujaribu apps hizo hapo chini ambazo zinafanyakazi sawa na apps ambazo nimezitaja kwenye list hapo juu.

Phone Check and Test
Price: To be announced

App hii ni kwa ajili wa watumiaji wa simu za Android na unaweza kufanya majaribio ya simu yako kwa undani na kujua simu yako ina tatizo gani. Unaweza kudownload app hii hapo juu au kupitia hapa.

Phone Doctor Plus
Price: Free

Phone Doctor pia ni app nyingine ambayo inaweza kusaidia kujaribu na kugundua matatizo mbalimbali ya simu yako. App hii pia ni kwaajili ya watumiaji wa simu za Android. Pakua app hii hapa au kupitia link hapo juu.

Kwa watumiaji wa simu za iPhone unaweza kupakua app ya TestM ambayo pengine ni app bora ya kugundua matatizo mbalimbali ya simu yako ya iPhone, unaweza kupakua app hiyo hapo juu au kwa kutumia link hapa.

Na hizo ndio njia ambazo unaweza kutumia kugundua matatizo mbalimbali ya smartphone yako. Kama kuna mahali umekwama au umeshindwa kutumia moja ya application hizo unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujifunza maujanja zaidi unaweza kubofya hapa.

6 comments
  1. Sim yangu Infinix hot 10i ila imegoma kufanya kazi finger print na kwenye security haipo kabisaaah.
    Je nifanyaje ili irudishe huduma hiyo?
    Ahsante

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use