Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Ndio Simu za Samsung Zitakazo Pata Toleo la Android Oreo

Simu za Samsung Galaxy zitakazo pata toleo jipya la Android Oreo 8.0
Samsung Galaxy Android Oreo Samsung Galaxy Android Oreo

Toleo jipya la Android Oreo au Android 8 lilitangazwa rasmi mwezi wa nane mwaka jana 2017, toka kipindi hicho hadi sasa baadhi ya kampuni za simu kama Sony, OnePlus na Nokia tayari zimesha anza kusambaza toleo hilo jipya.

Lakini kwa upande wa kampuni ya Samsung baadhi ya simu zimeonekana kupata toleo la majaribio huku watumiaji wengine wa simu za Samsung wakiwa wako gizani kuhusu kupata toleo hilo jipya. Sasa kupitia wataalamu wa teknolojia kwenye mtandao wa XDA wamefanikiwa kupata list ya simu za samsung ambazo zinasemekana zitapata toleo hilo jipya la Android Oreo ndani ya mwaka huu.

Advertisement

List hiyo ambayo imetokana na uchunguzi wa mafaili ndani ya mfumo wa Android Oreo wa majaribio kupitia simu ya Galaxy Note 8 unao onyesha simu hizo zitapata toleo hilo jipya ijapokuwa wataalam hao wanasema bado hawana uhakika kwa asilimia 100 kwani kunaweza kukawa na mabadiliko ya list hiyo muda wowote.

Kwa kuzingatia hayo hizi hapa ndio simu za Samsung zilizotajwa kwenye ukurasa wa XDA ambazo zinategemewa kupata toleo hilo jipya la Android Oreo 8.0

  • Samsung Galaxy A3 2017 (a3y17)
  • Samsung Galaxy A5 2017 (a5y17)
  • Samsung Galaxy A7 2017 (a7y17)
  • Samsung Galaxy A8 2016 SM-A810 (a8xe)
  • Samsung Galaxy A8 2018 (jackpotlte)
  • Samsung Galaxy A8+ 2018 (jackpot2lte)
  • Samsung Galaxy J3 2017 (j3y17)
  • Samsung Galaxy J5 2017 (j5y17)
  • Samsung Galaxy J7 2017 (j7y17)
  • Samsung Galaxy J7+ (jadelte)
  • Samsung Galaxy J7 Duos 2017 (j7duo)
  • Samsung Galaxy J7 Max (j7max)
  • Samsung Galaxy J7 Neo (j7velte)
  • Samsung Galaxy J7 Prime (j7popelte)
  • Samsung Galaxy Note FE (gracer)
  • Samsung Galaxy Note 8 (great)
  • Samsung Galaxy S7 (hero)
  • Samsung Galaxy S7 Edge (hero2)
  • Samsung Galaxy S8 Active (cruiserlte)
  • Samsung Galaxy S8 (dream)
  • Samsung Galaxy S8+ (dream2)
  • Samsung Galaxy W2018 (kellylte)

Kwa upande wa Tablet hizi ndio baadhi ya tablet mbazo nazo zinategemewa kupata toleo hilo jipya la Android Oreo ndani ya mwaka huu.

  • Samsung Galaxy Tab A 8.0 SM-T355 (gt58lte)
  • Samsung Galaxy Tab A 8.0 SM-T380/T385 2017 (gta2s)
  • Samsung Galaxy Tab A 10.1 SM-T580 (gtaxl)
  • Samsung Galaxy Tab Active 2 (gtactive2)
  • Samsung Galaxy Tab E 8.0 (gtesvelte)
  • Samsung Galaxy Tab S3 SM-T825 (gts3)

Kwa sasa hizo ndio baadhi ya simu za Samsung ambazo zimetajwa kwenye ukurasa huo ambazo zinasemekana zinaweza kupata mfumo mpya wa Android Oreo kabla ya kuisha mwaka huu. Lakini hata hivyo ripoti kutoka mitandao mbalimbali ya habari za teknolojia zinasema kuwa baadhi ya simu kama Samsung Galaxy C7 Pro, Samsung Galaxy C9 Pro, Samsung Galaxy J5 Pro, Samsung Galaxy J7 Pro pamoja na Samsung Galaxy S7 Active nazo zina tegemewa kupata mfumo huo.

Bado kampuni ya Samsung haijatoa list kamili ya simu ambazo zitapata mfumo huo mpya, lakini pengine tutegemee kuipata list hiyo hivi karibuni ukizingatia Samsung inajiandaa na uzinduzi wa Simu yake mpya ya Samsung Galaxy S9 hapo February 25 mwaka huu.

7 comments
  1. Kwa kweli kuna matoleo mengi sana ya simu janja lakini wengi tunaishia kuziangalia tu kufuatana na kipato chetu ni vigumu kuimiliki,watuletee nasi za bei ndogo za maujanja kwani nasi tunahitaji hayo.

  2. samsung s8 mpya naiuza kwa 600,000/= ninashida dukani ni 1600,000/= nimeitumia wiki 2 haina mchubuko ata mmoja hii ni mari halali pia ni unlocked to any network nitafute hapa bumbiscoo@gmail.com

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use