Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Spark 5 Pro Hapa Tanzania

Simu hii inakuja na memory kubwa pamoja na sifa nzuri zaidi
TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Spark 5 Pro Hapa Tanzania TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Spark 5 Pro Hapa Tanzania

Soko la simu limekuwa limekuwa na ushindani mkubwa na kupelekea makampuni ya simu kuja na mbinu mpya za kujizolea wateja. Tukiongelea makampuni pendwa ya simu hatuezi kuacha kuipongeza kampuni ya simu ya TECNO.

TECNO imekuwa kampuni bora kutokana na utofauti wa bidhaa zake Spark ya sasa hauezi ilinganisha na Spark ijayo ndivyo mawazo yangu yanavyoniambia.

Advertisement

Tunafahamu TECNO ina matoleo mbalimbali kama vile phantom, Camon, L series, Spark Series na mengineyo, na yote ni matoleo pendwa kutokana kuwa na sifa zenye kuvutia kama vile kamera nzuri, battery kubwa. lakini kati ya matoleo yote toleo la Spark limeonekana kupendwa sana labda hii ni kutokana muonekano mkubwa, utendaji maridhawa na bei isiyomuumiza mteja.

Pengine msomaji unaweza jiuliza kwanini nmeamua kuizungumzia TECNO au kama vijana wamjini mnasema kupiga debe hahahahahha, sawa basi acha nipige debe, leo nikiwa katika pita pita zangu mitaa ya kariakoo, katika duka Fulani hivi linafahamika kwa jina la Electrophones nimemsikia mteja mmoja akitamba TECNO Spark 5 Pro mbioni kuja mbona tutaepukana na ununuzi wa vimemory vilivyo jaa virusihayo ma GB 64 yatanitosha kabisa kuhifadhi mavideo na mapicha picha.

TECNO Kuzindua Simu Mpya ya Spark 5 Pro Hapa Tanzania

Mh nikiwa kama kijana mwenye kupenda utandawazi ndipo nilipo fukunyua kwenye ukurasa wa IG @tecnomobiletanzania na kukutana na picha ya Spark 5pro yenye sifa zenye kuonekanika kama kioo aina ya Dot in Display cha takribani nchi 6 au 7 si chini ya hapo, nyuma ikiwa na kamera 4(16MP+2MP+2MP+AI Lens) na MP8 za selfie. Kutokana na sifa hizo chache TECNO Spark 5pro ni mkali wa Spark zote za awali.

Ili kufahamu mengi zaidi tembelea mara kwa mara ukurasa wa Instagram @tecnomobiletanzania .

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use