Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus

Sifa hizi pia ni sifa za Samsung Galaxy S20 5G na Galaxy S20 Plus 5G
Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus

Baada ya Samsung kufanya uzinduzi wa simu zake mpya za Galaxy S20 na Galaxy Z Flip hapo jana, moja kwa moja karibu twende tukangalie sifa kamili pamoja na bei za simu hizi kwa hapa nchini Tanzania.

Kupitia makala hii tutaenda kuanza na simu za Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus alafu kwenye makala inayofuatia tuta angalia Galaxy S20 Ultra pamoja na Galaxy Z Flip. Kwa kuanza tuanze na muundo wa simu hizi, kama ilivyo tarajiwa Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus zimekuja na muundo unao fanana kidogo lakini kwa nyuma simu hizi zinakuja na muundo tofauti kabisa.

Advertisement

Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus

Samsung Galaxy S20 na S20 5G

Kwa mbele Galaxy S20 inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Dynamic AMOLED, huku kikiwa na uwezo mara mbili zaidi wa kufanya kazi kwa haraka pale mtu anapo gusa yani 2X capacitive touchscreen. Mbali na hayo kioo hicho kinakuja na uwezo wa resolution ya hadi pixel 1440 kwa 3200 pamoja na uwiano au aspect ratio ya 20:9.

Kwa juu ya kioo hicho kuna tundu la kamera ya mbele ambayo inakuja na uwezo wa Megapixel 10, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K. Kamera hiyo pia ina uwezo wa Auto-HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za Dual video call. Mbali na kamera hiyo, kwenye kioo hicho cha Galaxy S20 kunayo sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo inapatikana chini ya kioo.

Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus

Kwa nyuma S20 inakuja na muundo mpya kabisa huku kitu cha tofauti ikiwa ni kamera ambazo sasa zimewekwa kwenye mtindo mpya, kwa upande wa Galaxy S20 kamera hizo za nyuma zipo tatu huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni wide lens, na kamera nyingine mbili zikiwa ni Megapixel 64 ambayo ni telephoto lens na kamera ya mwisho ya Megapixel 12 ambayo yenyewe ni ultrawide lens. Kwa pamoja kamera zote zina uwezo wa kuchukua video za hadi 8K sawa na kusema simu hii ina uwezo wa kuchukua video za hadi 3240p@30fps.

Sifa za Samsung Galaxy S20 na S20 5G

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED 2X capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3200 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.73 GHz Mongoose M5 & 2×2.60 GHz Cortex-A76 & 4×2.0 GHz Cortex-A55) – Global.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 990 (7 nm+) – Global.
 • Uwezo wa GPU – Mali-G77 MP11 – Global.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya microSDXC.
 • Ukubwa wa RAM – GB 8 toleo la Galaxy S20 5G likiwa na GB 12.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 10 yenye f/2.2, 26mm (wide), 1/3.2″, 1.22µm, Dual Pixel PDAF na uwezo wa video hadi 2160p@30/60fps, 1080p@30fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12, yenye f/1.8, 26mm (wide), Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 64, yenye f/2.0, (telephoto), PDAF, OIS, 3x hybrid optical zoom, nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), AF, Super Steady video. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.2, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi za Cosmic Grey, Cloud Blue, na Cloud Pink.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM (kwa baadhi ya simu za USA na Canada), Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi yaani IP68 dust/water resistant (up to 1.5m for 30 mins).
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na zipo simu mbili moja yenye 4G na nyingine yenye 5G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint Chini ya Kioo (under display, ultrasonic)

Bei ya Samsung Galaxy S20 na S20 5G

Kwa upande wa bei ya Samsung Galaxy S20 na S20 5G zinategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu 2020 na bei ya simu hizi inategemewa kuanzia dollar za marekani $999 kwa toleo lenye 5G, hii ikiwa na sawa na takribani shilingi za kitanzania TZS 2,310,000 bila kodi. Kwa toleo lenye 4G, tegemea kupata simu hii kwa Euro €899 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania TZS 2,265,000 bila kodi. Galaxy S20 yenye 5G itakuwa inapatikana kwa baadhi ya nchi ambazo tayari zina 5G. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kwa Tanzania.

Samsung Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G

Kwa upande wa simu mpya ya Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G, simu hii haina tofauti sana na Galaxy S20 isipokuwa kioo cha Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G ni kikubwa zaidi na kamera za nyuma za Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G zimeongezwa na kuwa kamera nne. Pia vilevile Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G inakuja na battery kubwa zaidi.

Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus

Sifa za Samsung Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.7 chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED 2X capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3200 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.73 GHz Mongoose M5 & 2×2.60 GHz Cortex-A76 & 4×2.0 GHz Cortex-A55) – Global.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 990 (7 nm+) – Global.
 • Uwezo wa GPU – Mali-G77 MP11 – Global.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya microSDXC. Kuna toleo lingina la Galaxy S20 Plus 5G lenyewe linakuja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 128 na GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – GB 8 toleo la Galaxy S20 Plus 5G likiwa na GB 12
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 10 yenye f/2.2, 26mm (wide), 1/3.2″, 1.22µm, Dual Pixel PDAF na uwezo wa video hadi 2160p@30/60fps, 1080p@30fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12, yenye f/1.8, 26mm (wide), Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 64, yenye f/2.0, (telephoto), PDAF, OIS, 3x hybrid optical zoom, nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), AF, Super Steady video pamoja na Megapixel 0.3 ambayo ni TOF 3D, (depth). Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4500 mAh.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.2, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi za Cosmic Grey, Cloud Blue, na Cloud Pink.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM (kwa baadhi ya simu za USA na Canada), Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi yaani IP68 dust/water resistant (up to 1.5m for 30 mins).
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na zipo simu mbili moja yenye 4G na nyingine yenye 5G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint Chini ya Kioo (under display, ultrasonic).

Bei ya Samsung Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G

Kwa mujibu wa Samsung, Samsung Galaxy S20 Plus na S20 Plus 5G zinategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi wa tatu tarehe 8 mwaka huu 2020 na bei ya simu hizi inategemewa kuanzia Euro €999 kwa toleo lenye 4G, hii ikiwa na sawa na takribani shilingi za kitanzania TZS 2,520,000 bila kodi. Kwa toleo lenye 5G, tegemea kupata simu hii kwa dollar za marekani $1,199 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania TZS 2,770,000 bila kodi kwa toleo lenye GB 128 na Galaxy S20 yenye 5G yenye ukubwa wa GB 512 itakuwa inapatikana kwa dollar za marekani $1,299 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za kitanzania TZS 3,000,000 bila kodi.

Kumbuka bei hizi zinaweza kuongezeka kwa Tanzania kutokana na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha ikiwa pamoja na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use