Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 7.2 na Nokia 6.2

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya Nokia 7.2 na Nokia 6.2
Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 7.2 na Nokia 6.2 Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 7.2 na Nokia 6.2

Hapo jana kupitia mkutano wa IFA 2019 ambao unafanyika huko Berlin, Ujerumani. Kampuni ya Nokia imeongeza idadi ya simu zake zinazotumia Android kwa kuzindua simu mpya za Nokia 7.2 pamoja na Nokia 6.2. Simu hizi zinakuja zikiwa ni matoleo yanayo fanana kwa sifa na simu ya Nokia 8.1 ambayo ilizinduliwa hapo mwaka jana.

Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 7.2 na Nokia 6.2

Nokia 7.2

Advertisement

Tukianza na Nokia 7.2 simu hii inakuja na kioo cha inch 6.3 kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Kwa upande wa resolution simu hii inakuja na kioo chenye resolution ya hadi pixel 1080 x 2280 pamoja na uwiano wa 19 kwa 9 (ratio). Kwenye kioo hicho kwa juu simu hii inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 20 yenye uwezo wa kurekodi video hazi za pixel 1080p.

Kama ambavyo umeona kwenye video hapo juu, Nokia 7.2 inakuja na kamera tatu kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48 na kamera ya pili ikiwa na Megapixel 8 huku kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 5. Kamera zote kwa pamoja zinaweza kuchukua video za 4K pamoja na picha za hadi pixel 1080p, Hata hivyo kamera za simu hii zinasaidiwa na teknolojia kama Zeiss optics, panorama, HDR pamoja na Flash ya LED Flash.

Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 7.2 na Nokia 6.2

Kwa upande wa sifa za ndani Nokia 7.2 inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 660, processor ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 4 na GB 6. Nokia 7.2 pia inakuja na ROM au ukubwa wa ndani kati GB 64 na GB 128 ukubwa ambao unaweza kuongezwa kwa memory card hadi ya GB 512. Sifa nyingine za Nokia 7.2 ni kama zifuatazo.

Sifa za Nokia 7.2

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~400 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie), yenye Android One
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260) .
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 512.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili yenye ukubwa wa GB 64 na yenye ukubwa wa GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye f/2.0, 0.9µm.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.8, 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 5 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Zeiss optics, LED flash, panorama, na HDR.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa tatu za Cyan Green, Charcoal, na Ice .
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Nokia 7.2

Kwa upande wa bei Nokia imetangazwa simu hii inategemewa kupatikana baadae mwezi huu na itakuwa inapatikana kwa Euro €300 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 762,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kuongezeka kwa Tanzania.

Nokia 6.2

Kwa upande wa Nokia 6.2, simu hii haina tofauti na Nokia 7.2 kwa muundo ikiwa pamoja na asilimia kubwa ya sifa za simu hii. Kitu ambacho ni tofauti kwenye simu hii ni pamoja na bei, kamera za simu hii processor pamoja na RAM. Sifa nyingine pamoja na muundo vyote vinafanana.

Sifa za Nokia 6.2

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~400 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie), yenye Android One
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260) .
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 (14 nm).
 • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu tatu yenye ukubwa wa GB 32, GB 64 na yenye ukubwa wa GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, 0.9µm.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.8, 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 5 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Zeiss optics, LED flash, panorama, na HDR.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa mbili za Ceramic Black, na Ice .
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Nokia 6.2

Kwa upande wa bei Nokia 6.2 inatarajiwa kuuzwa kuanzia Euro 200 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 508,000 bila kodi. Kumbuka kwa Tanzania bei hii inaweza kubadilika kutokana na viwango vya kodi pamoja na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use