Seagate Yaleta Portable Hard Disk Kubwa Kuliko Zote ina 5TB

Kampuni ya Seagate imeleta hard disk kubwa kuliko zote duniani isoyo tumia umeme ya 5TB
Seagate Yaleta Portable Hard Disk Kubwa Kuliko Zote ina 5TB Seagate Yaleta Portable Hard Disk Kubwa Kuliko Zote ina 5TB

Siku ya jana kampuni maarufu kwa utengenezaji wa Hard Disk Seagate ilizindua hard disk yake ya Backup Plus Portable yenye ukubwa wa 5TB (Terabit 5), hard disk hiyo yenye ukubwa wa sawa na GB 5000 ndio hard disk pekee duniani yenye ukubwa huo lakini isiyotumia umeme bali waya wa kawaida wa USB 3.0.

Hard Disk hiyo ni portable kabisa ambayo ina fanana na ile ambayo inatumika kwenye laptop hivyo kufanya hard disk hii kuwa ya kwanza duniani kuwa na ukubwa wa 5TB, Hard disk hii kutoka Seagate ina uwezo wa kutuma files na data kwa kasi ya MB120 kwa sekunde hivyo usiwe na wasiwasi kuhusu hard disk hiyo kuchelewa kupokea data.

5tb

Advertisement

 

Vile vile hard disk hiyo imetengenezwa kwa kava lenye upana wa inch 0.8 sawa na millimeter 800 na itauzwa kwa dollar za marekani $189.99 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 450,000. Hard disk hii itanza kupatikana rasmi kuanzia mwezi ujao lakini unaweza kuangalia Hard disk hiyo kwenye tovuti Seagate.

Kwa Taarifa zaidi kuhusu Hard disk hii endelea kutembea Tanzania tech au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use