Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sasa Unaweza Kucheza Game za Playstation Kwenye Simu Yako

Sasa Unaweza Kucheza Game za Playstation Kwenye Simu Yako Sasa Unaweza Kucheza Game za Playstation Kwenye Simu Yako

Hadi kufikia mwaka 2016 utumiaji wa smartphone umeongezeka sana duniani kote na kampuni nyingi zinazo tengeneza video game zinaendelea kubadilisha mifumo yake na kuhamia kwenye mfumo wa smartphone. Hivi karibuni Kampuni inayotengeneza Playstation ijulikanayo kama Sony Computer Entertainment ilitangaza kubadilika kwa jina la kampuni hiyo na kuwa  Sony Interactive Entertainment Inc, hata hivyo kampuni hiyo ilitangaza kutengenezwa kwa sehemu mpya ya kampuni hiyo itakayoitwa  ForwardWorks.

Kampuni hiyo ya ForwardWorks ndio itakayokuwa ikitengeneza game hizo za playstation kwenye mfumo wa kidigitali yani kwenye mifumo kama ya smartphone, kampuni hiyo itaanza kufanya kazi rasmi tarehe 1 April 2016. Katika mkutano na waandishi wa habari Kampuni hiyo maarufu kwa utengenezaji wa Playstation games imesema watumiaji wa smartphone kwenye mfumo wa iOS pamoja na Android ndio watakao faidika na mfumo huo mpya utakao kuja hivi kaibuni.

Advertisement

Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kujaribu kuleta game za PlayStation kwenye mfumo wa Smartphone miaka michache iliyopita kampuni hiyo ilitoa simu maalumu kwaajili ya game hizo za playstation, hata hivyo simu hiyo haikupokelewa vizuri na watumiaji wa smartphone duniani. Wakati huu kampuni hii ikifanikiwa kuweka mfumo huo kwenye smartphone watumiaji wataweza ku-download games kutoka kwenye Play store Pamoja na App store.

12 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use