Jinsi ya Kudownload Profile Picture Yoyote Instagram

Utaweza kudownload profile picture yoyote hata kama akaunti ipo private
Jinsi ya Kudownload Profile Picture Yoyote Instagram Jinsi ya Kudownload Profile Picture Yoyote Instagram

Instagram ni moja kati ya mitandao mingi ya kijamii ambayo inatumiwa kwa wingi kwa sasa, lakini pia instagram ni sehemu muhimu ya kujitambulisha au kuonyesha wasifu wako binafsi wewe kama mfanyabiashara, mfanyakazi au mtumiaji yoyote wa kawaida.

Ni wazi kuwa Instagram imekuwa ikitumika kama kigezo cha kupata faida mbalimbali ikiwa pamoja na ajira au (endorsement) ambazo huwenda kufanya watu wengi kufanikiwa sana.

Kuliona hili leo nimekuja na njia ambayo itaweza kukusaidia wewe kama mtumiaji wa mtandao wa Instagram kuweza kudownload au kuangalia kwa ukaribu zaidi picha ya profile ya mtu yoyote kupitia mtandao wa Instagram.

Advertisement

Jinsi ya Kudownload Profile Picture Yoyote Instagram

Tumesha zoea kuwa picha za profile kwenye mtandao wa Instagram ni ndogo kiasi kwamba huwezi kuziangalia kwa ukaribu na pia huwezi kudownload picha hizo.

Kupitia njia hii nitakuonyesha njia ambayo ni rahisi na ambayo unaweza kutumia kudownload profile picture ya mtu yoyote kwenye mtandao wa Instagram. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye njia hii.

Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload install app hiyo kwenye simu yako kisha fungua na moja kwa moja fuata maelekezo hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kuinstall na kufungua app hii utaona sehemu ya kuandika ambapo unatakiwa kuandika jina au username ya profile ambayo unataka kudownload picha yake ya DP.

Jinsi ya Kudownload Profile Picture Yoyote Instagram

Baada ya kuandika jina la profile au username ya akaunti ambayo unataka kudownload profile picture moja kwa moja bofya sehemu ya Open Big Profile Photo.

Jinsi ya Kudownload Profile Picture Yoyote Instagram

Baada ya kubofya sehemu hiyo, moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa mwingine ambapo utaweza kuona profile picture moja kwa moja ikiwa kubwa kabisa.

Jinsi ya Kudownload Profile Picture Yoyote Instagram

Unaweza kuchagua Qualty ya picha kwa kuchagua kati ya size tatu chini mwisho wa ukurasa huo, pia unaweza kudownload picha hiyo na kuhifadhi moja kwa moja kwenye simu yako kwa kubofya kitufe cha download kilichopo upande wa kulia juu kwenye kona.

Kwa kufanya hatua hizi chache utakuwa umeweza kudownload profile picture ya mtu yoyote kwenye mtandao wa Instagram, kumbuka unaweza kudownload picha ya mtu yoyote hata kama akaunti hiyo ipo private. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kufanya matangazo kupitia akaunti yako ya Instagram kwa kutumia akaunti yako ya Mpesa. Pia unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza Profile picture bora.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use