Sasa Samsung Note 7 Ikiwa Imejaa Chaji ni Asilimia 60

Huu ndio muafaka wa Samsung kupitia simu zake za Note 7 baada ya Simu hizo kuonekana kulipuka mara kwa mara
note-7-chaji-ikijaa-itakua-asilima-60 note-7-chaji-ikijaa-itakua-asilima-60

Baada ya kampuni ya samsung kupata hasara kubwa kutokana na kulalamika kwa baadhi ya wateja wake duniani kutokana na kulipukiwa na simu hizo mpya za Note 7. Kampuni hiyo yenye makao makuu yake huko korea imetangaza kuwa imapata ufumbuzi wa muda kwa watumiaji ambao bado hawaja rudisha simu hizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya watu nchini marekani kuendelea kupeleka malalamiko kwenye kampuni hiyo ya samsung kwa sababu za kuendelea kulipuka kwa simu hizo ambazo kwa sasa zimeonekana kuwa ni hatari sana kutumia na watu mbalimbali duniani. Hata hivyo makala kutoka kwenye tovuti moja ya uingereza iliandika kuwa samsung imeamua kuchukua tahadhari kwa kutoa toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa simu hiyo ya Note 7 ambapo mfumo huo mpya utakua ukizuia simu hiyo kujaa chaji zaidi ya asilimia 60%.

Hata hivyo bado haijaeleweka kuwa (update) hizo zitalazimishwa kwenye simu hizo ama laa!. Pia habari kutoka katika tovuti hiyo ziliendelea kusema kua katika miji ya Ufaransa Samsung imesha sema kua itazima simu hizo moja kwa moja mpaka hapo itakapo tangaza tena baada ya simu hizo kuwa salama.

Advertisement

Bado tatizo la simu hizo za Samsung Galaxy Note 7 linaendela kuipa hasara kampuni hiyo kutokana na kuendelea kushuka kwa hisa za kampuni hiyo kila siku, lakini pia kampuni hiyo imeendela kusisitiza kuwa bado inaendelea kupambana na tatizo hilo ili kuruhusu simu zake hizo za Note 7 kurudi tena sokoni kwa awamu ya pili zikiwa salama na bora zaidi.

Endelea kufuatilia swala hili kila siku kwa kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use