Sehemu Bora za Kupata Mkopo wa Smartphone

Hizi hapa sehemu bora za kupata mkopo wa kununua smartphone
Sehemu Bora za Kupata Mkopo wa Smartphone Sehemu Bora za Kupata Mkopo wa Smartphone

Kuwa na smartphone ni muhimu sana katika maisha ya kisasa. Smartphone inakusaidia kuwasiliana na watu, kutafuta habari, na hata kupata huduma za kifedha na hata huduma nyingine za muhimu kama bima na nyingine.

Hata hivyo, si kila mtu anaweza kumudu kununua simu ya mkononi, hasa smartphone. Kwa bahati nzuri, kuna njia za kupata smartphone simu kwa kukopa. Kupitia makala hii nimekuleta sehemu bora ambazo unaweza kupata simu au smartphone kwa kukopa.

Y9 Microfinance

Y9 Microfinance ni kampuni inayotoa huduma za kifedha nchini Tanzania. Kampuni hii inatoa mikopo ya haraka na rahisi mbali ya hayo kampuni hii pia inatoa mikopo kwa watu ambao wanataka kununua simu au smartphone kwa kulipa kidogo kidogo.

Advertisement

Sehemu Bora za Kupata Mkopo wa Smartphone

Unaweza kupata mkopo wa simu ya hadi Tsh 500,000 utalipia simu hiyo kila siku kuanzia utakapo chukua simu hiyo. Unahitaji tu kuwa na kitambulisho cha Taifa na data nyingine za muhimu kuthibitisha uwezo wako wa kulipa mkopo.

Fahamu zaidi Jinsi ya Kujiunga na Y9 Microfinance Hapa

Tigo Tanzania

Tigo Tanzania ni moja ya kampuni kubwa za simu nchini Tanzania. Kampuni hii inatoa huduma za kifedha kwa wateja wake, ikiwa ni pamoja na mikopo ya simu za mkononi. Unaweza kupata mkopo wa hadi smartphone ya hadi TZS 500,000 kulingana na aina ya uwezo wako wa kifedha kupitia Tigo Pesa. Unahitaji tu kuwa mteja wa Tigo Pesa, kuwa na kitambulisho cha taifa na kuthibitisha uwezo wako wa kulipa mkopo.

Sehemu Bora za Kupata Mkopo wa Smartphone

Kama unataka kujiunga na huduma hii unatakiwa kubofya *147*00# kisha chagua namba 9, kisha chagua 3 Duka la Simu kisha chagua huduma kulingana na mahitaji yako.

Vodacom Tanzania

Sehemu Bora za Kupata Mkopo wa Smartphone

Vodacom Tanzania ni kampuni nyingine kubwa ya simu nchini Tanzania. Kampuni hii pia inatoa mikopo ya kununua simu ya smartphone kwa wateja wake. Unaweza kupata mkopo wa smartphone wa hadi Tsh 500,000. Kama ilivyo kwa kampuni ya Tigo, ili kujiunga na huduma ya mkopo wa simu kwa Vodacom unahitaji kuwa mteja wa huduma ya M-Pesa kutoka Vodacom na unahitaji kuwa na kitambulisho cha taifa na kuthibitisha uwezo wako wa kulipa mkopo.

Jinsi ya kujiunga piga *150*00# kisha chagua sehemu ya Mikopo.

Easy Buy Tanzania

Easy Buy by Tecno Tanzania ni huduma mpya ya kununua simu za Tecno kwa mkopo. Huduma hii inaruhusu wateja kununua simu za Tecno kwa awamu, badala ya kulipa fedha taslimu kwa mara moja. Unaweza kupata simu ya Tecno kwa mkopo. Unahitaji tu kujaza fomu na kuthibitisha uwezo wako wa kulipa mkopo ikiwa pamoja na vigezo vingine kama kitambulisho cha taifa na mahitaji mengine ya muhimu.

Sehemu Bora za Kupata Mkopo wa Smartphone

Kwa hiyo, kama unataka kununua smartphone lakini huna fedha taslimu, unaweza kupata mkopo kutoka kwa kampuni za kifedha kama Y9 Microfinance, Tigo Tanzania, na Vodacom Tanzania. Pia unaweza kutumia huduma ya Easy Buy by Tecno Tanzania kununua simu ya Tecno kwa mkopo.

Kumbuka kufuata vigezo na masharti ya ukopaji na pia hakikisha unaweza kuthibitisha uwezo wako wa kulipa mkopo kabla ya kuchukua mkopo wowote.

2 comments
 1. Yapo makampuni mengine makubwa na madogo madogo na hata maduka yanatoa mikopo ya simu kwa masharti tofauti tofauti.
  Mfano:
  Mysol(awali Mobisol)
  Sunking
  Simu safi
  N.k

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use