Video: Aina Mpya ya Material yenye Uwezo wa Kujiunga

Wanasayansi wagundua aina mpya ya material yenye uwezo wa kujiunga
Kujiunga Kujiunga

Wote tunajua kuwa teknolojia inakimbia kwa kasi sana pengine kuliko hata watu wanayoitumia, kuthibitisha hilo wtafiti kutoka chuo cha University of California, Riverside marekani wamefanikiwa kugundua aina mpya ya materia ambayo inaweza kujiunga pale inapo chanika au kupata tatizo lolote.

Mbali na uwezo wake wa kujiunga material hii inauwezo wa kutanuka na kuwa kwenye ukubwa au urefu mara 50 zaidi kulinganisha na kiasi cha material hiyo. Aitha katika taarifa ya uzinduzi wa metiral hiyo kiongozi wa wagunduzi hao alisema kuwa ametengeneza material hiyo kutokana na filamu na muigizaji wa movie ya X-Man ajulikanae kama Wolverine. mgunduzi huyo anae itwa Chao Wang mwenye Ph.D aliendelea kusema kuwa alikuwa anatamani sana kuponya dunia kwa kuzuia baadhi ya vitu kaharibika au kuvunjiaka na ndipo alipo fanikiwa zoezi hilo kupitia chuo cha University of California.

Advertisement

Hata hivyo material hiyo imeanza kufanyiwa utafiti ili kutengeneza battery za simu aina ya lithium ion ili pale unapo iangusha iweze kujijenga yenye na kusababisha simu yako kudumu na chaji pamoja na battery. Material hiyo inasemekana kutengenezwa kwaajili ya kutengeneza simu zenye uwezo wa kujiunga zenyewe hivyo labda tusubiri kidogo pengine tunaweza kutumia simu za aina hiyo kwenye miaka ya karibuni.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use