App za Kutengeneza Matangazo Bora ya Instagram na FB

Utaweza kuvutia wateja zaidi kwa matangazo bora kupitia Instagram na Facebook
App za Kutengeneza Matangazo Bora ya Instagram na FB App za Kutengeneza Matangazo Bora ya Instagram na FB

Ni ukweli usio pingika kuwa Instagram ni moja kati ya sehemu bora sana za kupata wateja wapya, hii inatokana na wingi wa watu wanaotuma mtandao huo ambao hadi sasa inasemekana mtandao huo unao zaidi ya watumiaji bilioni 1 kila mwezi, namba hii inaenda ikiongezeka kwa kasi.

Sasa kupitia zaidi ya watumiaji bilioni 1 kwa mwezi kote duniani, ni wazi kuwa kutafuta masoko kupitia instagram ni jambo la muhimu kwa biashara ya aina yoyote.

Kuliona hilo leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia sana kuweza kutengeneza matangazo bora ya Instagram ambayo yanaweza kuvutia watu wengi sana kwenye biashara yako pale unapo amua kutangaza biashara yako kupitia Instagram.

Advertisement

Tofauti na makala nyingine ambazo huwa ni ndefu sana, makala ya leo sio ndefu kwani njia hii pia sio njia ndefu hata kidogo, na mtu yoyote anaweza kufanya hatua hizi na kuvutia watu zaidi pale anapofanya matangazo kwenye akaunti yake.

Basi bila kupoteza muda moja kwa moja twende nikuonyeshe njia hizi rahisi na za haraka ambazo unaweza kutumia. Kwa kuanza hakikisha unayo Internet kwenye simu yako kisha pakua app hapo chini.

Matangazo Kupitia Story

Kama unataka kutangaza kupitia Instagram Stories basi app ya Story Maker Pro ni app bora sana kwako.

Uzuri wa app hii ni kuwa inakuja na uwezo wa kusaidia kutengeneza stories kupitia picha na video ambazo tayari zimesha andaliwa na wewe unaweza kuedit tu na kusave kwenye simu yako na moja kwa moja unaweza stories hizo kwenye mtandao wako wa instagram au mitandao mingine.

Tofauti na toleo la kawaida ambalo lipo Play Store, toleo la pro linakupa uwezo wa kutengeneza stories bila matangazo bila kuwa na kikomo na bila kutengeneza akaunti ya aina yoyote.

Kama unafikiria kutengeneza post bora za Stories kupitia mtandao wa Instagram na hata Facebook basi app hii ni muhimu kuwa nayo kuanzia siku ya leo.

Download Hapa

Matangazo Kwenye Post za Kawaida

App za Kutengeneza Matangazo Bora ya Instagram na FB

Kama unataka kutengeneza matangazo ikiwa pamoja na post mbalimbali za instagram na hata mitandao mingine kwa urahisi na haraka basi app hii ya Poster Maker Flyer ni app bora sana kwako.

App hii kama ilivyo app hapo juu hii pia inakupa uwezo wa kutengeneza Post kutoka kwenye picha ambazo tayari zimesha andaliwa.

Unachofanya wewe ni kuedit moja ya picha ambayo unataka kutumia na moja kwa moja utaweza kusave kwenye simu yako na kutangaza biashara yako kwa urahisi na haraka.

Ni rahisi sana kutumia na pia utaweza kutengeneza post bora ambazo zitavutia wateja wengi kwenye biashara yako kupitia mtandao wa Instagram.

Download Hapa

Kama bado hujui jinsi ya kufanya matangazo kupitia mtandao wa Instagram basi hakikisha una angalia video hapo chini kujua hatua kwa hatua jinsi ya kufanya.

Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kutangaza biashara yako kupitia Instagram, na pia utakuwa unaweza kutengeneza matangazo bora ya Instagram ambayo yatakusaidia kuvutia wateja zaidi kwenye akaunti yako.

Kama unataka msaada zaidi unaweza kutuandikia sehemu ya kupitia maoni hapo chini, kwa maujanja zaidi ya Instagram unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuweka theme kupitia sehemu ya DM.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use