Kutana na Masako Bibi wa Miaka 81 Alie Tengeneza App ya iOS

Bibi wa kwanza duniani kutengeneza App ya iOS
Masako Wakamiya Masako Wakamiya

Mara nyingi watu hudhani kuwa kuwa mzee kunakufanya huwe ni mtu ambae huwezi tena kufuatilia mambo pamoja na kujifunza mambo mapya hayo yamepigwa vikali na Octogenarian Masako Wakamiya bibi wa miaka 80 mwenye makazi yeke huko nchini japan.

Masako aliamua kutengeneza programu (App) ya mfumo wa iOS ili kusaidia watu wa nchini kweke yani japan kujua namna bora ya kuweka wadoli ambao hutumiaka sana na wajapan kwenye sherehe mbalimbali za wakazi wa nchi ya japan. Masako alitengeneza app yake hiyo aliyo ipa jina la Hinadan ambalo limetokana na maneno ya kijapan ya “hina” lenye maana ya mdoli na “dan” lenye maana ya mstari wa vitu vilivyoko sawa.

Masako Wakamiya ni mmoja kati ya bibi wa chache ambao bado wananguvu ya kujifunza mengi pamoja na kufundisha mengi sana kwenye jamii ya japan pamoja na dunia nzima kwa ujumla, Masako amekua ni mfano wa kuikwa hata kwenye mikutano TED ambayo alishwahi kufanya kwenye miaka ya nyuma, unaweza kuangalia show ya mkutano huo hapa.

Advertisement

App ya Hinadan sasa inapatikana kupitia App Store unaweza kudownload app hiyo hapo chini ili kuangalia utalamu wa bibi huyu ambaye anaonyesha kwa watu kuwa bado dunia ina mambo mengi sana ya kujifunza hata kama una miaka 81.

‎hinadan
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha hupitwi kwa kudownload App ya Tanzania Tech kupitia play store na unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania tech kupitia mtandao wa Youtube.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use