Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Telegram Yaja na Maboresho Kwenye App Zake za Android na iOS

Sasa utaweza kuchati na watu waliopo karibu na eneo ulilopo
Telegram Yaja na Maboresho Kwenye App Zake za Android na iOS Telegram Yaja na Maboresho Kwenye App Zake za Android na iOS

Telegram ni moja kati ya App nzuri sana za kuchat, kama wewe ni mkimbizi kutoka app ya WhatsApp basi ni vyema kujaribu kambi ya Telegram kwani nakuhakikishia hutoweza tena kurudi kwenye app yako ya WhatsApp kutokana na uzuri wa app ya Telegram.

Kwa kuanza labda ni kujulishe kuwa, hivi karibuni telegram imefanya mabadiliko kwenye programu yake ya kuchat na imeongeza sehemu mpya kadhaa ambazo zinafanya uweze kutumia app hiyo kwa urahisi zaidi.

Advertisement

Chat na Watu Walio Kuzunguka

Kupitia toleo jipya la Telegram 5.8.0, Telegram imeongeza njia mpya ambayo unaweza kutumia kuchat na watu walipo karibu na eneo ulilopo, unachotakiwa kufanya ni kuwasha sehemu ya location kisha bofya sehemu ya Contact kisha bofya sehemu iliyo andikwa People Nearby, baada ya hapo kama kuna mtu ambaye yupo karibu na wewe na kafungua ukurasa huo kama wewe basi utawea kuona moja kwa moja kupitia kwenye sehemu hiyo.

Telegram Yaja na Maboresho Kwenye App Zake za Android na iOS

Mbali na hayo Telegram pia inakuja na sehemu mpya ya kutengeneza Group ambalo litakuwa na watu waliopo kwenye eneo ulilopo. Sehemu hii inapatikana pia kwa chini kwenye sehemu ya People Nearby.

Telegram Yaja na Maboresho Kwenye App Zake za Android na iOS

Mbali na sehemu hizo, Pia telegram imeongeza sehemu mpya ambayo unaweza kuitumia kumpa mtu mwingine admin wa group fulani. Sehemu hii inafanya kazi pale tu unapo mpa mtu group ambaye yupo tayari ndani ya group hilo. Kwa mujibu wa Telegram hayo ndio maboresho mapya yaliyoletwa kwenye app ya Telegram, kama bado huna app ya Telegram unaweza kudownload app hiyo kupitia link hapo chini.

Unknown app
Price: Free

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use