Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Hii hapa njia rahisi na bora ya ku-edit PDF kwa kutumia kompyuta
Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows) Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Kama wewe ni mfutiliaji wa tovuti ya Tanzania tech ni wazi kuwa unajua jinsi ya ku-edit PDF kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kama bado hujui jinsi ya kufanya hivyo nakushauri kusoma makala hiyo kwanza na uhakika itakusaidia sana.

Baada ya kujaribu njia hiyo lakini unaona kuwa njia ya kutumia kompyuta ni njia bora kwako basi endelea kwa kusoma makala hii. Kumbuka njia hii ni maalum kwa watumiaji wa kompyuta za Windows hivyo ni muhimu kuwa na kompyuta yenye mfumo wa Windows kabla ya kuendelea.

Baada ya kuhakikisha unatumia mfumo wa Windows, moja kwa moja tembelea tovuti hapo chini kisha download programu hiyo na install kwenye kompyuta yako. Baada ya kuinstall moja kwa moja endelea kwa kufuata maelekezo hapo chini.

Advertisement

Download Programu Hapa

Baada ya kuinstall programu hiyo vizuri, moja kwa moja nenda kwenye dokmenti yoyote ya PDF unayotaka ku-edit, kisha moja kwa moja fungua dokmenti hiyo kwa kutumia programu hiyo uliyo download hapo juu.

Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Baada ya hapo moja kwa moja sogeza kasa au mouse yako kwenye neno lolote au picha iliyoko kwenye PDF unayotaka ku-edit. Bofya mara moja kuchagua sehemu ya neno unalotaka kuedit.

Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Kisha baada ya hapo bofya mara mbili kwenye mstari au sehemu ya maneno au picha unayotaka ku-edit.

Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Kama unavyoweza kuona, sasa utaweza kubadilisha sehemu hiyo ya maneno iliyopo kwenye pdf, na kizuri ni kuwa mwandiko ulipo hauto tofautiana na muandiko unao andika kwa muda huo.

Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Mbali na hayo pia utaweza ku-edit picha iliyopo kwenye PDF hii ikiwa ni pamoja na logo na kila kutu kama vile sign pamoja na kila kitu kilichopo kwenye PDF.

Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Utaweza kubadilisha logo kwa kuchagua logo husika kisha delete au badilisha kwa kuchagua logo nyingine kutoka kwenye kompyuta yako. Baada ya ku-edit chochote hakikisha unakumbuka kusave kwa kuchagua sehemu ya File kisha bofya Save.

Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Kwa kufanya hivyo moja kwa moja utakuwa umeweza ku-edit PDF kwa urahisi kwa kutumia kompyuta yako ya Windows. Kumbuka kama unataka ku-edit PDF kwa kutumia kompyuta yenye mfumo wa MacOS, kwa sasa bado tuna angalia njia bora zaidi hivyo endelea kutembelea Tanzania tech kila siku kujifunza zaidi.

Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku, pia unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuandika CV ikiwa pamoja na mifano ya CV zaidi ya 200 ambayo unaweza kutumia kuandika CV yako. Hadi siku nyingine endelea kutembelea Tanzania tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use