Jiandae na Simu Mpya ya Infinix Note 10 Hapa Tanzania

Simu hii inakuja na sifa bora kama chipset ya Media Helio G95 yenye nguvu zaidi
Jiandae na Simu Mpya ya Infinix Note 10 Hapa Tanzania Jiandae na Simu Mpya ya Infinix Note 10 Hapa Tanzania

Nilishawahi kuandika awali kuhusu ujio wa Infinix NOTE 10 na kutaja baadhi ya sifa zake. katika pitapita zangu za mitandaoni nimeona tovuti mbalimbali zikiendelea kuzungumzia ujio wa simu hiyo na baadhi ya sifa kuu zikitajwa kuwa ni Chipset ya Mediatek Helio G95 na GB8 Rom huku picha zinazoendelea kusambaa mitandaoni zikionyesha muonekano wa simu hiyo ukiwa na camera 4 nyuma.

Kupitia picha hizo inaonyesha moja ya rangi ya Infinix NOTE 10 ni zambarau ambayo ni sawa na rangi mpya ya zambarau ya iphone 12 na iphone 12 min. Maelezo ya tovuti ya Price in Tanzania  yana onyesha Infinix NOTE 10 ni simu iliyo jaa sifa za kisasa zenye kuhitajika katika soko la simu kama vile chaji ya type C na teknolojia ya X-charge 33W kazi yake kuu ni kuchaji battery la simu kwa haraka.

Infinix NOTE 10 inatia hamasa ya kutaka kufahamu sifa zake zote kiundani zaidi lakini kupitia sifa hizo chache hapo juu inahashiria mabadiliko makubwa ya toleo la Infinix NOTE.

Advertisement

Tujikumbushe toleo la NOTE kwa kampuni ya Infinix. Toleo la Infinix NOTE linawalenga zaidi wafanyakazi wa maofisini, wafanyabiashara na mtu yoyote mwenye matumizi makubwa ya simu kama videographer, wapenzi wa games na mwanafunzi pia mwenye kuitumia simu yake kama sehemu yakujisomea.

Tafadhali endelea kutembelea https://www.infinixmobility.com.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use