Instagram Kuja na Sehemu Mpya ya Portrait Mode ‘Focus’

Sehemu hiyo itakusaidia kupiga picha nzuri kupitia Instagram
Instagram Kuja na Sehemu Mpya ya Portrait Mode ‘Focus’ Instagram Kuja na Sehemu Mpya ya Portrait Mode ‘Focus’

Hivi karibuni habari kuhusu mtandao wa instagram zinasema, kwa sasa instagram inafanyia kazi sehemu mpya ya Portrait Mode ambayo itakuwa inaitwa Focus. Kwa mujibu wa msemaji wa Instagram sehemu hiyo itaweza kukusaidia kuchukua picha zinazo onekana vizuri zaidi.

Sehemu ya Portrait Mode iko kwenye kamera za simu nyingi za siku hizi, sehemu hii inakusaidia kuweza kuchukua picha ya eneo la mbele la kitu unachotaka kupiga picha huku kwa nyuma kukiwa hakuonekani vizuri, yaani kunakuwa na ukungu flani au kwa kitaalam (blur). Sasa sehemu hiyo mpya ya Focus kwenye instagram ambayo inakuja na teknolojia hiyo ya Portrait Mode itakusaidia kuweza kupiga picha za aina hiyo.

Kwa sasa bado haijajulikana ni lini sehemu hii itawezeshwa kwenye programu za Instagram, lakini tayari instagram ime – thibitisha kwa waandishi wa tovuti ya TechCrunch kuwa ni kweli inafanya majaribio ya sehemu hiyo.

Advertisement

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use