Ifahamu Vizuri Apple TV

AppleTV AppleTV

TV ni moja kati ya sehemu muhimu sana katika jamii zetu kwani pale tunapo jikusanya na ndugu jamaa na marafiki kuangalia filamu, vipindi mbalimbali au michezo ndipo hapo tunapojenga zaidi umoja na mshikamano baina yetu, lakini kutokana na technolojia kukua kila siku zipo TV nyingi mbalimbali duniani zenye ubora mbalimbali zinazo fanya ubadilishe kabisa jinsi unavyofikiria Technolojia ya TV kwa miaka inayokuja.

Apple TV ni technolojia iliyokwepo karibia miaka tisa sasa toka ilipo zinduliwa mwaka 2007, technolojia hii mpya imekuwepo kwa muda sana lakini cha aajabu ni watu wachache sana wanaitumia technolojia hii mpya kutizama michezo, habari pamoja na matamsha mbalimbali.

Advertisement

Apple TV ni mfumo ambao naweza kusema binafsi kuwa ni moja kati ya tecknolojia ambayo inatakiwa kwa sasa duniani kwani ulimwengu unahamia kwenye Digital yani nikiwa na maana kuwa Hakuna haja tena ya kuwa na Tecknolojia ya zamani kwani  sasa kuna tecknolojia mpya zenye uwezo mkubwa kuliko hata tecknolojia hizo za zamani tunazo zishikilia sana . Apple TV imebadilisha kabisa muonekano wa TV na kukuletea uwezo zaidi ya ule uliokua unaujua, kama wewe ni mpenzi wa Smart TV Apple TV ndiyo tv yako TV hii ina uwezo wa kuifadi application ambazo zitafanya uone TV yako kuwa ni ya kisasa na ya maana zaidi.

Unaweza pia kucheza game mbalimbali pia kutizama Filamu mpya na mambo mengine mengi moja kwa moja katika TV yako hii ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuzipakua game hizo moja kwa moja kutoka iTune Store, pia TV hii itakuwezasha kutumia application kama zile za Siri na mambo mengine mengi ama kwa hakika Apple TV ni ulimwengu mpya wa TV. Kujua zaidi kuhusu Apple TV angalia video hiyo apple juu pia unaweza uka bofya hapo chini kusoma zaidi kuhusu TV hiyo ya Kisasa.

Bofya Hapa Kusoma Zaidi Hapa

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use