Hizi Ndio Simu za Kwanza Kabisa za Android Pamoja na iPhone

Kutokana na historia kubwa ya Smartphone hebu tujue kidogo Android na iPhone
Simu ya kwanza ya Android na Iphone Simu ya kwanza ya Android na Iphone

Android na iPhone ni simu ambazo kiukweli kwa sasa ndio simu zilizopo kwenye chati na hii ni kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya simu hizo pamoja na watumiaji wake, lakini hebu ngoja turudi nyuma kidogo na tuangalie mwanzo wa simu hizi na mahali zilipo tokea.

  • Simu ya Kwanza ya Android

Tukianza kwa upande wa Android, simu ya kwanza ilizinduliwa mwezi September 2008 na simu hii ilitoka chini ya kampuni ya HTC kwa ushirikiano na kampuni ya Google pamoja na kampuni ya huduma za simu ya T Mobile, ambapo kwa pamoja walikuja na simu hiyo ya kwanza iliyokuwa inaitwa HTC Dream au T-Mobile G1.

Advertisement

Kwa kipindi hicho simu hii ilikuwa ni moja ya simu za kisasa kabisa na kwa upande wangu nakumbuka kutumia simu hii na ukweli ilikuwa ni simu ya thamani kubwa pamoja na sifa za kipekee sana. Simu hii ya T Mobile G1 ilikuwa na kioo cha inch 3.2 ambacho kilikuwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya TFT capacitive touchscreen yenye uwezo wa kuonyesha rangi elfu 65.

Simu hii pia ilikuwa ikitumia processor ya Qualcomm MSM7201A ambayo ilikuwa na nguvu ya MHz 528 pamoja na GPU ya Adreno 130. Kwa upande wa ukubwa wa ndani simu hii ilikuwa na ukubwa wa ndani wa MB 256 huku ikisaidiwa na RAM ya MB 192. Mbali na hayo simu hii ilikuwa na uwezo wa kusoma memory card hadi ya GB 16.

Kwa upande wa kamera simu hii ilikuwa na kamera moja tu ya nyuma iliyokuwa na Megapixel 3.15 ambayo ilikuwa na teknolojia ya autofocus, pamoja na uwezo wa kurekodi video. Battery ya simu hii ilikuwa ni ndogo sana na kwa upande wangu ilikuwa ni simu inayoisha chaji kwa haraka sana ikiwa na uwezo wa Li-Ion 1150 mAh huku ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji masaa 5 pekee. Kwa upande wa mfumo simu hii ilikua inatumia mfumo wa kwanza wa Android uliokuwa unaitwa Android 1.6 (Donut).

  • Simu ya Kwanza ya iPhone

Kwa upande wa iphone, simu ya kwanza ya iPhone ilizinduliwa tarehe 9 January 2007 huko nchini marekani na ilizinduliwa chini ya kampuni ya Apple Inc kwa ushirikiano na kampuni ya huduma za simu ya AT&T, simu hii ilikuwa ya kwanza kabisa kuwa na mfumo bora wa muziki kutokana na kuwa na mfumo wa iPod ndani yake.

Kwa upande wangu nakumbuka simu hii ilikuwa ni moja kati ya simu za bei ghali sana na ni watu wachache sana walikuwa nazo, simu hii nakumbuka ilijulikana sana kwa vitu vitatu vikubwa, kitu cha kwanza ilikuwa ni uwezo wake wa muziki, simu hii ilikuwa iko vizuri sana kwa upande wa muziki na kutokana na muziki ulikuwa adimu sana kipindi hicho basi ukiwa na simu hii ni kama unamiliki radio kubwa yenye uwezo mkubwa wa muziki.

Kitu cha pili kilichokuwa kinavutia watu wengi kwenye simu hii ni aina yake ya kufunga na kufungua ambayo ilikuwa inaitwa “slide to unlock” sehemu hii ilikuwa maarufu sana na ilikuwa ni kitu cha kushangaza kidogo ukimuona mtu anafungua simu hiyo kwa kupapasa kidole kwenye kioo cha simu hiyo.

Kwa upande mwingine pia simu hii ya kwanza ya iPhone ilikuwa maarufu kwa kuwa na ukubwa wa ndani mkubwa pamoja na sifa zingine kama kioo cha inch 3.5 kilichokuwa kimetengezwa kwa teknolojia ya TFT capacitive touchscreen pamoja na uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16. Upande wa processor iPhone ilikuwa na uwezo wa 412 MHz pamoja na GPU iliyokuwa inaitwa PowerVR MBX.

Simu hii ilikuwa na ukubwa wa ndani wa GB 4, GB 8 pamoja na GB 16 na ilikuwa haina sehemu ya kuweka memory card. Upande wa kamera simu hii ilikuwa na kamera moja ya Megapixel 2 tu na ilikuwa haina uwezo wa kuchukua video. Na kwa upande wa battery simu hii ilikuwa inadumu na chaji kuliko android na ilikua inatumia battery ya Li-Ion iliyokuwa na uwezo wa kudumu hadi masaa 8.

  • Hitimisho

Simu hizi zote mbili ni baba wa smartphone na kwa mujibu wa mitandao mbambali, kutokana na kuwai kutoka kwa iphone kabla ya Android wengi wanasema simu ya kwanza ya Android ilitengenezwa kwa kunakili muundo wa simu ya kwanza ya iPhone lakini mimi binafsi ninashaka kuhusu hili, je wewe unaonaje tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use