Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Heri ya Mwaka Mpya 2021

Tunakutakia heri ya mwaka mpya, mwaka ukawe wa baraka kwako na mafanikio zaidi.
Heri ya Mwaka Mpya 2021 Heri ya Mwaka Mpya 2021

Kwanza ni wazi kuwa tuna kila haja ya kushukuru Mungu kwa kutupa nafasi nyingine ya kuona mwaka mpya 2021.

Pili ni wazi kuwa Tanzania tech inakuwa kwa kasi sana na kwa hili napenda kuchukua nafasi hii kushukuru sana kwako wewe msomaji wetu kwani umekuwa nasi kwa mwaka mzima na umetupa support ya nguvu sana!

Advertisement

Kitu cha muhimu tunaomba uendelee kuwa nasi kwani tumekuandalia mambo mengi mazuri ambayo najua yanaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine hasa kwenye ulimwengu huu wa teknolojia.

Mabadiliko Machache

Ukweli ni kwamba maendeleo huja na mabadiliko na kuna wakati mabadiliko yanaweza kuwa yanaumiza lakini kwa upande wa mabadiliko haya natumaini wote tutaweza kufurahia.

Siku za karibuni tumebadilisha app ya Tanzania tech kutoka kwenye kipengele cha “News & Magazine” kwenda kwenye kipengele cha “Education”. Hii ni hatua ya kwanza ya kubadilisha tovuti ya Tanzania tech kuwa tovuti ya elimu zaidi ya maswala ya teknolojia kutoka kwenye tovuti ya “Habari za Teknolojia” pekee.

Heri ya Mwaka Mpya 2021

Hii haina maana kwamba taarifa za muhimu hautazipata kupitia Tanzania tech “Hapana”, utaendelea kupata taarifa mbalimbali za teknolojia lakini sio kila habari ya teknolojia utaipa. Hapo tutakuwa tunakuleta habari za muhimu pekee ambazo tunaona kweli zina uzito na umuhimu wa wewe kujua.

Habari nyingine zote za teknolojia zitaendelea kuwepo kama kawaida kupitia mitandao yetu ya kijamii ya InstagramFacebookTwitter na Telegram. Kama bado hujajiunga nasi hakikisha unafanya hivyo ili kupata habari zote mpya za Teknolojia.

Nini Kitakuwa kwenye Tanzania Tech

Kuanzia hivi karibuni, kama ilivyo kuwa kwa siku za mwishoni mwa mwaka 2020, utaendelea kuona makala zaidi za jinsi ya kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia.

Utaendelea kupata makala zenye kufundisha kutumia teknolojia mbalimbali kama vile teknolojia ya smartphone, tovuti mbalimbali bila kusahau njia mbalimbali za kutengeneza pesa mtandaoni.

Heri ya Mwaka Mpya 2021

Mbali na hayo pia utapata makala za video zenye kuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kufanya mambo mbalimbali yanayo husiana na teknolojia moja kwa moja kupitia channel yetu ya YouTube.

Pia tunategemea kuzindua bidhaa zetu mbalimbali ambazo naamini zinaweza kusaidia watu wengi kufanya mambo mengi kwa urahisi na haraka.

Kama wewe ni mpenzi wa Tanzania tech naamini mwaka 2021 utakuwa mwaka bora zaidi kwako kwani tuta kuletea mambo mengi mazuri ambayo najua yataongeza ujuzi, elimu na kipato kwako wewe mtumiaji wa mitandao na teknolojia kwa ujumla.

Yaliyopo Sasa

Kama umekuwa mtembeleaji wa tovuti ya Tanzania tech ni wazi kuwa una fahamu kuhusu sehemu mpya ya “Group chat”. Sehemu hii sasa inapatikana kwenye app ya Tanzania tech na unaweza kuwa mmoja wa washirika wetu kwa kujaribu sehemu hiyo.

Heri ya Mwaka Mpya 2021

Kwa sasa sehemu hii bado ipo kwenye hatua za majaribio na tunaendelea kuboresha sehemu hii kadri muda unavyokwenda, kitu cha msingi ni vizuri kuwa mmoja wa watakao jaribu sehemu hii ili tuweze kujua ni sehemu gani ya kuboresha zaidi.

Unaweza kupata sehemu hii kupitia app ya Tanzania tech kwenye soko la Play Store, unaweza kudownload app yetu sasa kama bado hauna kwenye simu yako, pia kama unayo unaweza kusasisha (Update) kwenye toleo jipya ili kupata sehemu hii.

Mwisho

Mwisho kabisa napenda kushukuru sana kwa kuwa nasi kwa kipindi chote cha mwaka mzima. Pia napenda kukutakia mwaka mpya wenye mafanikio na baraka zaidi. Mungu akubariki sana!.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use