Facebook Yaomba Radhi kwa Kutuma Ujumbe wa Safe Check kwa Nchi Zingine

Facebook Yaomba Radhi kwa Kutuma Ujumbe wa Safe Check kwa Nchi Zingine Facebook Yaomba Radhi kwa Kutuma Ujumbe wa Safe Check kwa Nchi Zingine

Facebook imeomba radhi hivi karibuni kwa kukosea kutuma ujumbe mfupi wa maneno uliokua na kusudi la kufaamisha ndugu na jamaa katika mtandao wa facebook kama uko salama, haya yalitokea jumapili ya tarehe 27 march 2016 baada ya tukio la bomu lililotokea lahore katika mji wa Pakistan.

Shambulio hilo lilotokea siku ya jana ndio liliosabibisha Facebook kuanza kutuma meseji hizo kwa watumiaji wake ili kusaidia kujua kama wako salama, meseji hizi ni moja kati ya mpango maalum ulioanzishwa na facebook kusaidia kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa wanaotumia mtandao wa facebook kama uko salama. Mpango huu unatumika sana kwenye nchi za barani ulaya na asia hata hivyo facebook hutuma ujumbe huu kwa nchi iliyoadhiriwa tu na sii vinginevyo.

Siku ya jana mfumo huo wa kutuma ujumbe mfupi ulipata itilafu na kutuma ujumbe huo hata kwa nchi ambazo hazija adhiriwa na tukio lililotokea hapo jana, baadhi ya nchi zilizopoeka ujumbe huo ni kama United States na united kingdom pamoja na nchi zingine mbalimbali.

Advertisement

Hii sio mara ya kwanza kwa mfumo huo kukosea kutuma ujumbe huo ujulikanao kama “Safe Check” mwaka 2015 mwenyekiti mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg aliomba msamaa kwa watumiaji wa mtandao huo wa facebook baada ya mfumo huo kukosea kutuma tena ujumbe baada ya mlipuko uliotokea Beirut huko Lebanon na kuuwa watu 43.

Ujumbe uliotumwa ni kama huo unaonekana hapo chini kwenye picha

facebook messege

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use