‘Discover People’ Njia Mpya ya Kupata Marafiki Facebook

Hii Ndio Njia Mpya ya Kukusaidia Kupata Marafiki Kwenye Facebook
Facebook Discover People Facebook Discover People

Kama list yako ya marafiki kupitia facebook ni ndogo usijali facebook imesikia kilio chako, hivi karibuni facebook imeleta sehemu mpya ya kusaidia kupata marafiki ijulikanayo kama “Discover People”.

Sehemu hiyo mpya inatarajiwa kuja hivi karibuni kwenye programu za facebook za Android pamoja na iOS, Kujua jinsi inavyofanya kazi mtumiaji anatakiwa kubofya sehemu ya option iliyoko upande wa kulia kisha utachagua sehemu iliyoandikwa Discover People. Baada ya hapo utaletewa sehemu maalum ambayo itakusaidia kujiunga na watu wa karibu yako, kwa mfano kama wewe ulienda kwenye event flani na watu wengine wote walioenda kwenye event hiyo mtaunganishwa pamoja ili kujiunga na kuwa marafiki.

Sehemu hiyo haita onyesha marafiki ambao tayari umekua marafiki nao, hiyo ni ili kukusaidia kugundua marafiki wapya kwa haraka. Sehemu hiyo bado inaendelea kutoka kwenye programu za iOS pamoja na Android hivyo kama bado hujapata sehemu hiyo angalia update za programu hiyo na hakikisha una update kupata sehemu hiyo mpya ya Discover People.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia Download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kupata habari za teknolojia haraka pindi tu zitakapo toka. Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa njia ya Video.

7 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use