Blackview P10000 Pro Simu Yenye Battery Kubwa Kuliko Zote

Simu hii ya Blackview inauwezo wa kudumu na chaji kwa wiki nzima
Blackview P10000 Pro Blackview P10000 Pro

Tatizo kubwa la simu nyingi za mkononi ni Battery, tunajua simu mbalimbali zenye uwezo mkubwa wa Battery ikiwa pamoja na uwezo mkubwa wa kutunza chaji. Lakini simu zote hizo hazifananishwi na simu hii mpya ya Blackview P10000 Pro, simu hii inauwezo wa kudumu na chaji hadi siku 7 yaani wiki moja, vievile kama huitumii mara kwa mara simu hii inauwezo wa kudumu na chaji hadi siku 50.

Kinacho ipa simu hii uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu kiasi hicho ni Battery yake kubwa yenye uwezo wa 11,000mAh, uwezo ambao haujawahi kutokea kwenye simu ya mkononi. Kiasi hichi cha battery ni kikubwa hata kuliko baadhi ya laptop au kompyuta mpakato.

Advertisement

Mbali na uwezo wa battery ya simu hii, kama ambavyo ungedhani Battery hii inakuja na teknolojia ya Quick Charge ambayo inauwezo wa kujaza simu hii chaji kutoka asilimia 0 hadi asilimia 100 kwa muda wa masaa mawili na dakika 25.

Japokua simu hii sio pekee yenye battery kubwa, lakini hii ndio simu ya kwanza yenye uwezo wa Battery ya 11,000mAh. Mwaka jana kampuni yingine ya nchini china inayojulikana kama Oukitel ilizindua simu za K10000 na K10000 Pro, ambazo zenyewe zilikuwa na uwezo wa Battery kubwa ya 10,000mAh ambayo yenyewe ilikuwa na uwezo wa kuchaji simu zingine.

Kwa upande wa sifa za simu hii ya Blackview P10000 Pro, ukiachana na battery simu hii inakuja na sifa za kawaida za kioo cha inch 5.5 chenye teknolojia ya Full HD pamoja na ulinzi wa kioo cha Gorilla Glass. Kwa upande wa processor simu hii inakuja na processor ya octa-core MediaTek MT6750T processor yenye uwezo wa 1.5 GHz. Kwa upande wa RAM simu hii inakuja na RAM ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32. Kwa upande wa kamera simu hii ya Blackview P10000 Pro inakuja na kamera nne kwa ujumla ikiwa na kamera mbili kwa mbele zenye Megapixel 13 na Kamera mbili kwa nyuma zenye Megapixel 16.

Kama umeipenda simu hii na unaitaka, unaweza kununua kupitia tovuti ya Alibaba kwa bei rahisi ya punguzo ya dollar za marekani Tsh $197.79 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 450,000. Unaweza kununua kwa kubofya hapo chini.

Nunua Blackview P10000 Pro

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use