Hii Ndio Memory Kadi Kubwa Kuliko Zote Duniani Inayo 1TB

1TB SDXC kutoka kampuni ya SanDisk ndio memory kadi kubwa kuliko zote dunia na imezinduliwa hivi karibuni
Memory Kadi Memory Kadi

Kampuni maarufu ya Western Digital Corporation (NASDAQ: WDC) ambayo ni maarufu sana kwa utengenezaji wa vifaa vya kuhifadhi data, hivi karibuni imezindua memory kadi kubwa kuliko zote duniani ambayo ukubwa wa 1TB (Terabyte).

Kwa mujibu wa Tovuti ya SanDisk ambayo iko chini ya Western Digital, memory kadi hiyo  ambayo itazinduliwa chini ya Jina la SanDisk 1TB terabyte (TB) SDXC imetengenezwa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya watu mbalimbali kutokana na kukuwa kwa teknolojia mpya za 4k pamoja na 8k. Akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano wa Photokina uliofanyika tarehe 20 Sep 2016, huko Cologne Germany mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya West Digital Mr Dinesh Bahal alisema kuwa wanafurahi sana kuweza kufanikiwa kusukuma mipaka ya teknolojia kwani Memory kadi hiyo itakua ni mwazo mzuri wa mwaka unaokuja pamoja na miaka mingine inayokuja ambapo wanaamini kuwa kwao ni miaka ya uvumbuzi wa kiteknolojia.

https://www.youtube.com/watch?v=kOAxy7H4Xek

Advertisement

Hata hivyo mpaka sasa kampuni hiyo bado haijaweka wazi kuwa ni lini memory kadi hiyo itaanza kuuzwa rasmi au itauzwa kwa kiwango gani. Hata hivyo kutokana na bei ya memory kadi ya GB512 iliyo zinduliwa na kampuni hiyo hapo mwaka 2014 kuwa na Bei ya dollar za marekani $800 inawezekana kabisa bei ya memory kadi hiyo ya 1TB kuwa bei zaidi ya dollar za marekani $800 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,749,880.00 kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya tarehe 22-09-2016.

Unaweza kuendelea kupata habari za memory kadi hiyo kwa kuendelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use