LG Yazindua Laptop Mpya za LG Gram Inch 17 na LG Gram 14

Hizi ndio Laptop mpya kutoka LG zenye uzito mdogo kuliko laptop nyingine za LG
LG Yazindua Laptop Mpya za LG Gram Inch 17 na LG Gram 14 LG Yazindua Laptop Mpya za LG Gram Inch 17 na LG Gram 14

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki ya LG hivi karibuni imetangaza kuzindua laptop zake mpya za LG Gram ya Inch 17 pamoja na LG Gram ya Inch 14. LG Gram ya inch 17 inakuja na uwezo wa processor ya 8th Gen Core i7 processor (8565U) yenye uwezo wa SSD ya GB 512 na RAM ya GB 16. Laptop hii pia inatajwa kuwa ni laptop nyepesi huku ikiwa na uzito wa pound 3 tu ambayo ni sawa na kilo 1.3.

LG Yazindua Laptop Mpya za LG Gram Inch 17 na LG Gram 14

Laptop hii inakuja na kioo cha inch 17 ambacho pia kina kuja na resolution ya 2560 x 1600, laptop hii pia inakuja na sehemu ya fingerprint pamoja na battery ambayo LG inadai inauwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 19.5 pale inapochajiwa mara moja. Sifa nyingine za LG Gram ya inch 17 ni kama zifuatazo.

Advertisement

Sifa za LG Gram Inch 17 (2019)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 17 chenye teknolojia ya LCD WQXGA IPS, sRGB 96% pamoja na resolution ya 2560 x 1600 pixels, na uwiano wa 16:10 ratio.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Windows 10
  • Uwezo wa Processor – Core i7 processor.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Intel 8th Gen Intel® Core™ Processor.
  • Uwezo wa GPU – Intel UHD Graphics.
  • Uwezo wa Hard Disk / SSD – 256GB / 512GB (M.2 Slot)
  • Ukubwa wa RAM –  8GB / 16GB (DDR4, 1 on board + 1 slot)
  • Uwezo wa Battery – Battery ya 72Wh yenye uwezo wa kudumu na chaji hadi masaa 19.5.
  • Viunganishi – USB 3.1 Type-C (Thunderbolt™ 3 Option), USB 3.1 x 3, Dual Mic, HDMI, microSD, HP/Mic Out (Combo).
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za White na Dark Silver.
  • Mengineyo – Inakuja na Keyboard yenye kuwaka taa (Backlit Keyboard, 98 keys).
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint.

Kwa upande wa LG Gram ya Inch 14 yenyewe inakuja na teknolojia ya 2 in 1 huku ikiwa na uwezo wa kuwa tablet na Laptop. Kioo chake cha inch 14 kinakuja na teknolojia ya touchscreen ambacho pia kina uwezo wa kutumika kwa kutumia kalamu maalum. Laptop hii nayo inasemekana ni nyepesi zaidi kwani inakuja na uzito wa pound 2 tu ambayo ni sawa na kilo 0.907185.

LG Yazindua Laptop Mpya za LG Gram Inch 17 na LG Gram 14

Laptop hii nayo inakuja na processor ya 8th Gen Intel Core i7 processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 16 pamoja na hard disk / SSD ya GB 512. Kwa mujibu wa LG, laptop hii inakuja na battery ya 72Wh ambayo inauwezo wa kudumu na chaji hadi masaa 21 inapo chajiwa mara moja. Sifa nyingine za laptop hii ya LG Gram ya inch 14 ni kama zifuatazo.

Sifa za Laptop ya LG Gram ya Inch 14 (2019)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 14 chenye teknolojia ya FULL HD Touch IPS Display, Corning® Gorilla® Glass 5 pamoja na resolution ya 1920 x 1080 pixel, na uwiano wa 16:9 ratio.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Windows 10 Home
  • Uwezo wa Processor – Core i7 processor.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Intel 8th Gen Intel® Core™ Processor.
  • Uwezo wa GPU – Intel UHD Graphics.
  • Uwezo wa Hard Disk / SSD – 256GB / 512GB (M.2 Slot)
  • Ukubwa wa RAM –  8GB / 16GB (DDR4, 1 on board + 1 slot)
  • Uwezo wa Battery – Battery ya 72Wh yenye uwezo wa kudumu na chaji hadi masaa 19.5.
  • Viunganishi – USB 3.1 Type-C (Thunderbolt™ 3 Option), USB 3.1 x 3, Dual Mic, HDMI, microSD, HP/Mic Out (Combo).
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Dark Silver.
  • Mengineyo – Inakuja na Keyboard yenye kuwaka taa (Backlit Keyboard, 98 keys), inakuja na kalamu maalum.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint.

Bei ya LG Gram Inch 17 na LG Gram Inch 14

Kwa upande wa bei LG Gram ya inch 17 yenyewe inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $1,699.99 ambayo ni sawa na Tsh 3,911,000 bila kodi na kwa upande wa Kenya ni Ksh 175,000 bila kodi. LG Gram ya Inch 14 ambayo pia ni 2 in 1, bado haijatangazwa bei yake hivyo endelea kutembelea ukurasa huu tutakuhabarisha pindi tu bei ya laptop hiyo itakapo tangazwa. Laptop zote zinategemewa kupatikana rasmi kupitia mkutano wa CES 2019.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use