Adobe Yatambulisha App Mpya Kwaajili ya Ku-Scan Document

Kampuni ya adobe kupitia programu zake za adobe leo imetambulisha app mpya
Adobe Scan Adobe Scan

Wote tunaijua kampuni ya Adobe kutokana na kazi zake na kwa wengine tunaijua kampuni hii kutokana na kutoa ajira kupitia programu zake maarufu kwaajili ya utengenezaji picha, video pamoja na ubunifu wa tovuti, kuongezea kwenye mkusanyiko wa programu zake hivi karibuni adobe imeleta programu mpya kwaajili ya mifumo ya iOS na Android.

Programu hiyo mpya imezinduliwa rasmi hapo jana na imetengenezwa maalum kwaajili ya kurahisisha kuscan docemet zako zilizoko kwenye mfumo wa karatasi kuja kwenye mfumo wa kidigital, yote hayo kwa kuwezeshwa na kamera ya simu ya mkononi (smartphone). Kwa sasa programu hizo zinapatikana rasmi kwenye mifumo yote ya simu yaani iOS pamoja na Android, hivyo unaweza kudownload app hizo kupitia link hizo hapo chini.

  • Adobe Scan – Kwa Mfumo wa iOS
  • Adobe Scan – Kwa Mfumo wa Android

Kumbuka programu hizi ni bure kabisa huna haja ya kununua lakini inakubidi kuwa na akaunti ya Adobe ili kuweza kuingia ndani ya app hiyo, ili kujiunga unaweza kutengeneza akaunti moja kwa moja kwenye app hiyo ni rahisi sana hivyo hakuna wasiwasi.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video. 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use