in

Jinsi ya Kupata Namba za Simu za Zamani Ulizopoteza

Njia hii ni bora na unaweza kupata namba zote za simu za zamani zilizopotea

Jinsi ya Kupata Namba za Simu za Zamani Ulizopoteza

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamepoteza namba za simu za watu ambao hapo zamani ulikuwa na namba zao basi njia hii itakusaidia sana.

Kupitia njia hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia mtandao wa Facebook kuweza kupata namba za simu za zamani ambazo umepoteza, njia hii ni rahisi sana na mtu yoyote mwenye akaunti ya facebook anaweza kufanya.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sasa basi kwa kuanza unatakiwa kuwa umeingia kwenye akaunti yako ya Facebook kwa kutumia kivinjari (browser) yako kama vile Google Chrome au Opera Mini. Hakikisha una switch kwenye akaunti yako binafsi kama unatumia akaunti zaidi ya moja au kama una page mbalimbali.

Jinsi ya Kupata Namba za Simu za Zamani Ulizopoteza

Baada ya kumaliza hatua za kuswitch kwenda kwenye akaunti yako binafsi moja kwa moja bofya link hapo chini.

Tembelea Facebook Hapa

Jinsi ya Kupata Namba za Simu za Zamani Ulizopoteza

Baada ya kubofya link hiyo utapelekwa kwenye ukurasa wa Facebook ambao utakuwa unafanana kabisa na ukurasa kwenye picha hapo juu.

Utaweza kuona namba na majina zikiwa zimefichwa na ili kuweza kuona namba ya mtu bofya namba husika na moja kwa moja utaletewa namba kamili.

Kwa kufanya hatua hizo utaweza kupata namba za simu za watu ambao ulipotezana nao kupitia mtandao wa Facebook. Kumbuka unaweza kupata namba zote ikiwa pamoja na majina kamili jinsi ambayo ulikuwa umesave hapo awali ulipo poteza.

Kumbuka njia hii inafanya kazi kwa simu yoyote au kompyuta na unaweza kupata namba kwa urahisi na haraka bila kujali aina ya kifaa au simu unayo tumia.

Amani Joseph

Jinsi ya Kupata Namba za Simu za Zamani Ulizopoteza

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments

  1. Kupitia makala hii nimechoka nimechoka na nilichokiona, namba za watu tangu 2015 nimezikuta huko na sikujua nitazipata wapi maana Google contact walipoteza namba zangu zote kwa email asante kaka ila changamoto kuzipakua sasa