Infinix Yashinda Tuzo za Design Kimataifa (2023)

Tuzo za Usanifu wa DNA Paris huheshimu miundo katika taaluma za Usanifu
Infinix Yashinda Tuzo za Design Kimataifa (2023) Infinix Yashinda Tuzo za Design Kimataifa (2023)

Kampuni ya simu za mkononi Infinix yenye makao makuu nchini Hong Kong yatwaa ushindi katika usanifu wa bidhaa/vyombo vya habari na electroniki za nyumbani nchini Paris.

Infinix Tanzania kupitia kurasa zake za mtandao wa kijamii @infinixmobiletz imepost video kusherehekea ushindi huo uliopatikana kupitia simu mahiri aina ya Infinix NOTE 30.

Infinix NOTE 30 imetengenezwa kwa umahiri mkubwa kutumika kwajili ya mawasiliano ya mitandao ya simu. Umbo lake ni jembamba lililonyooka na lisilo na mambo mengi, muonekano wa nyuma umetawaliwa na kioo pamoja na leather ubunifu umeipa kampuni hii ushindi mkubwa.

Advertisement

 
 
 
 
 
View this post on Instagram
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

A post shared by InfinixMobileTanzania (@infinixmobiletz)

Infinix NOTE 30 si simu ya muda mrefu sokoni lakini tangu kuingia kwake hajaacha kuwa gumzo imekuwa ikivutia sana mashabiki na teknolojia ya fast charge ambapo ukichaji kwa dakika 30 inajaza battery kwa 75% na ukichaji kwa dakika 5 unaweza cheza games, kusikiliza Music na kuwatch movie kwa muda wa masaa mawili.

Ikiwa inafanya vyema katika soko la simu nchini lakini pia imejitwalia heshima kubwa ya kimataifa DNA. Tuzo za Usanifu wa DNA Paris huheshimu miundo katika taaluma za Usanifu, Usanifu wa Ndani, Usanifu wa Mandhari, Usanifu wa Picha na Muundo wa Bidhaa unaowatunuku wabunifu bora zaidi duniani kote.

Hongera nyingi sana kwa ushindi huu mkubwa kwa Kampuni hii na wadau kindakindaki wa simu za Infinix.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use