Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako

Mambo haya ndio baadhi ya mambo yanayo ongoza kuharibu battery za simu
Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako

Battery ni chanzo cha wewe kuweza kusoma makala, hii ndio maana leo nimeona tuongelee kidogo kuhusu battery ili kusudi uweze kuendelea kusoma makala za Tanzania Tech kila siku bila kuwa na wasiwasi wa battery ya smartphone yako.

Kupitia makala hii nitaenda kukujuza mambo kadhaa ambayo ni adui mkubwa wa battery ya simu yako, mambo ambayo yanaweza kufanya battery ya simu yako kuharibika au kuisha chaji kwa haraka mara kwa mara. Hakikisha unajitahidi sana kuacha au kutofanya mambo haya hasa kama unatumia smartphone.

Joto Kali Kwenye Simu

Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako

Advertisement

Joto kali ni moja kati ya ishara kubwa sana ya simu yako kufanya kazi kupita uwezo wake, lakini mbali na hayo joto kali ni adui namba moja wa battery ya simu yako kwani hii husababisha battery kuisha kwa haraka na wakati mwingine battery kuharibika kabisa ndani ya muda mfupi.

Hakikisha unapotumia simu yako haipati joto kali sana kwani mara nyingine hii inaweza kuwa na madhara ya moja kwa moja kama vile battery kulipuka au mambo mengine kama hayo.

Pia mara nyingi simu hutoa kiasi kikubwa cha miozi au SAR pale simu inapokuwa inapata joto kali sana, hivyo simu inapokuwa na joto kali sana ni adui hata kwa afya yako mwenyewe hivyo akikisha una jitahidi kutumia simu ikiwa haipo chaji, pia chaji simu yako ikiwa iko kwenye sehemu yenye hewa na jitahidi kupunguza matumizi pale unapochaji simu yako.

Power Bank

Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao mara nyingi wapo barabarani basi ni wazi unatumia Power Bank, kama unatumia vifaa hivyo basi ni vyema kuongeza uangalifu hasa pale unapoamua kununua power bank kwaajili ya simu yako.

Mara nyingi power bank zisizo na ubora huwa na mtindo wa kuharibu batter ya simu yako kwa haraka sana hasa inapokuwa kwenye kifaa hicho kwa muda mrefu.

Hivyo basi jitahidi sana kununua power bank yenye uwezo mzuri ambayo itakuwa na uwezo wa kuchaji simu yako wa haraka na kwa muda mfupi ili kuepuka simu yako kuungana na power bank kwa muda mrefu. Jitahidi kununua power bank yenye uwezo wa 2A ambayo hii ni sawa na AC adapter.

Kuchaji Huku Unatumia Simu

Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako

Kuchaji simu pia ni soma ambalo nadhani tunahitaji kuongelea hapa Tanzania Tech, lakini kwa siku ya leo ni vyema ufahamu kuwa asilimia kubwa ya watu wanachaji simu zao vibaya na hii kusababisha battery za simu kuharibika ndani ya muda mfupi sana.

Baadhi ya battery za simu ni rahisi sana kuharibika kwa mtindo mbaya wa kuchaji hivyo ni muhimu kuwa makini.

Hakikisha usitumie simu yako huku unachaji kwa muda mrefu, kwani hii ni hatua ambayo inaharibu sana battery ya simu yako, kama una haraka sana ya kutumia simu yako washa flight mode pale unapokuwa unachaji simu yako itajaa chaji kwa haraka na utaweza kutumia ndani ya muda mfupi.

Vilevile hakikisha unaondoa kava la simu yako ambalo limebana sana simu yako pale unapochaji simu yako kwani hii huweza kusababisha joto kwenye simu yako, kitu ambacho ni adui wa kwanza wa battery ya simu yako.

Kutumia Chaja Isiyo Sahihi

Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako

Baada ya kuongezeka kwa tamaduni ya kampuni za simu kuuza simu bila kuweka chaja kwenye box Imekuwa ni kawaida watu kutumia chaji yoyote kuchaji smartphone bila kuwaza aina ya chaji inayotumia, mara nyingi watu hujali zaidi kuhusu simu zao kupata chaji kuliko kuangalia aina ya chaja inyotumika kuchaji simu husika.

Mara nyingi kuna sababu za kampuni za simu kutengeneza chaja maalum kwa ajili ya smartphone husika kwani teknolojia iliyotumika kutengeneza chaja hizo inakuwa inafanana au inaendana na smartphone husika, pia chaja hiyo inakuwa imepimwa na kuonekana kuwa na uwezo wa kutosha wa kuchaji simu husika.

Hivyo ni vizuri kununua chaja ya simu husika kwani japo kuwa kampuni za simu sasa zinauza simu bila chaja ila unaweza kununua chaja ya simu husika kutoka duka la simu ulipo nunulia simu yako.

Na hayo ndio baadhi tu ya mambo ambayo ni muhimu kuzingatia sana kama unataka kuendelea kusoma tovuti ya Tanzania Tech bila kuwa na wasiwasi wa battery ya simu yako kisha kila siku kwa haraka. Kumbuka bado yapo mambo mengi sana ya kulinda simu yako hivyo unaweza kusoma hapa kujua mambo mengine yanayoweza kusaidia simu yako zaidi.

6 comments
  1. msaada nataka kujua kuhusu blog ya swagpay ivi ni kweli inalipa au ni matapeli maana naona inalipa kiasi kikubwa sana cha pesa 10$ kwa referral na 2$ kwa kila atakae klick link naomba msaada wako bro

  2. iv kuweka cimu yak kwa mda mrefu kwenye charge inapelekea kuharibika kwa battery?

    1. Inategemea na aina ya simu, lakini simu za siku hizi nyingi zinakuja na kifaa maalum ambacho husaidia kuzuia chaji isiendelee kuingia kama simu imejaa chaji. Lakini ni wazo zuri kuchaji simu kwa muda maalum.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use