Jinsi ya Kutuma Meseji WhatsApp Bila Kusave Namba

Huna haja ya kuandika link au kuinstall app ya aina yoyote
Jinsi ya Kutuma Meseji WhatsApp Bila Kusave Namba Jinsi ya Kutuma Meseji WhatsApp Bila Kusave Namba

WhatsApp ni mojawapo ya programu kubwa za ujumbe na inahudumia zaidi ya watumiaji bilioni 2 ulimwenguni kote. Mbali na hayo ili kuwaleta watu pamoja, WhatsApp imeanzisha vipengele kama vile WhatsApp Communities, kushiriki mahali ulipo na hata uwezo wa kujitumia ujumbe.

Lakini hata hivyo inawezekana kuna baadhi ya sehemu kwenye programu ya WahtsApp ambazo pengine ulikuwa huzijui au hazija tangazwa na hivyo kupelekea watu wengi kuto kufahamu.

Moja ya sehemu hiyo ni pamoja na njia mpya ya kutuma meseji bila kuhifadhi namba ya mtu kwenye simu yako.

Advertisement

Njia hii ni rahisi na huna haja ya kuinstall programu yoyote kwenye simu yako, na kizuri zaidi ni kuwa njia hii inafanya kazi kwa watumiaji wa Android pamoja na iOS.

Jinsi ya Kutuma Ujumbe WhatsApp Bila Kusave Namba

Kwa kuanza hakikisha programu yako ya WhatsApp ipo kwenye toleo jipya kisha, hakikisha kipengelea cha “Message yourself” kinapatikana kwenye programu hiyo.

Baada ya hapo fungua sehemu yenye jina lako na neno You, kisha andika namba ya mtu unayetaka kumtumia ujumbe wa WhatsApp.

Jinsi ya Kutuma Meseji WhatsApp Bila Kusave Namba

Huna haja ya kuandika +255 unaweza kuandika namba pekee mfano 0712123456, baada ya hapo tuma meseji hiyo au jitumie meseji hiyo ambayo itakua na namba pekee.

Jinsi ya Kutuma Meseji WhatsApp Bila Kusave Namba

Baada ya hapo bofya, au click namba iliyopo kwenye meseji na kwa kufanya hivyo itafunguka menu yenye sehemu iliyoandikwa Chat with 0712123456 bofya hapo na utaweza kuaza kuchati na mtu bila kuifadhi namba ya mtu kwenye simu yako.

Jinsi ya Kutuma Meseji WhatsApp Bila Kusave Namba

Njia hii ni bora sana na nimekuwa nikutumia mara kwa mara hasa kwa kuwasiliana na biashara kutokea mtandaoni. Kama unataka kujifunza zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech pia pakua app ya Tanzania Tech kuhakikisha hupitwi na maujanja mbalimbali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use