in

Download Picha Zote, Profile, Stories na Video Instagram

Pia utaweza kucopy description ya picha pamoja na hashtag kwa urahisi

Download Picha Zote, Profile, Stories na Video Instagram0:49

Kama kwa namna yoyote umekuwa ukitaka kudownload picha zote zilizopo kwenye mtandao wa instagram ikiwa pamoja na profile picture za watu, video, stories, reels na kila kitu ikiwa pamoja na kuondoa matangazo na mambo mengine mengi basi unasoma makala sahihi.

Kupitia njia hii na uhakika utaweza kuendelea kuitumia kwa muda wote ambao utakuwa unataka kupakua picha au hata profile picture.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kizuri zaidi ni kuwa njia hii itakupa hadi uwezo wa kucopy description au comment yoyote ambayo unataka kwenye mtandao wa Instagram, basi bila kupoteza muda twende kwenye njia hii.

Kwa kuanza pengine nikwambie app hii ni copy ya instagram na inakupa uwezo wa kupakua picha, video au kuangalia akaunti ambazo zipo “private” moja kwa moja.

Unachotakiwa kufanya ni kupakua app hiyo kisha moja kwa moja install kwenye simu yako ya Android, baada ya hapo hakikisha unatumia username na password ya akaunti ambayo sio muhimu sana kwako ikiwezekana tengeneza akaunti mpya.

Kisha ingia kwenye app hii na akaunti yako hiyo mpya na sasa utaweza kufanya mambo mbalimbali kwa urahisi na haraka. App hii mimi natumia kwa muda sasa na ukweli its the best app for me.

Download Picha Zote, Profile, Stories na Video Instagram

Kama unavyoweza kuona utaweza kupakua reels, stories, video au picha yoyote kwa kubofya kitufe cha download. Pia utaweza kuangalia na kudownload profile picture ya mtu yoyote kwa ukubwa kwa kushikilia profile picture hiyo.

Download Picha Zote, Profile, Stories na Video Instagram

Mbali na hayo utaweza kufanya mambo mengine mengi zaidi, kama kucopy description iliyoko kwenye picha yoyote au video ikiwa pamoja na kwenye stories. Hii itakupa urahisi wa kunakili hashtag.

Download Picha Zote, Profile, Stories na Video Instagram

Kimsingi yapo mambo mengi sana unaweza kufanya na app hii, Jaribu app hii na uhakika utakuwa unaitumia kila mara unapotaka kudownload picha au video yoyote kwenye mtandao wa Instagram.

Download Mbadala wa Instagram Hapa

Na hiyo ndio njia bora na rahisi ya kupakua picha zote za profile picture, stories, reels na video yoyote kwenye mtandao wa Instagram.

Kama unataka kujua jinsi ya kupakua video za mtandao wa TikTok bila kuwa na logo au watermark ya mwenye video unaweza kusoma makala iliyopita hapa.

Amani Joseph

Download Picha Zote, Profile, Stories na Video Instagram

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kujua Mafile Yanayochukua Nafasi Kubwa (Kompyuta)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.