in

Jinsi ya Kuficha Mafile ya Android kwa Kutumia Calculator

Weka data zako salama kwa kuficha mafile yako ya muhimu kwa kutumia calculator

ficha kwa calculator

Ni wazi kuwa smartphone ni simu binafsi kwa kila mmoja wetu, lakini kuna wakati inakuwa ni ngumu kuzuia watu wengine kutumia simu yako ndio maana leo nimekuletea njia hii ya kuficha mafile ya simu yako ya Android kwa kutumia Calculator.

Njia hii ni bora sana kwani inakusaidia kuficha vitu vya muhimu kama vile picha na vitu vingine ambavyo ungependa kuzuia watu wengine kuwaza kuona.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hivyo basi kwa kufuata maelezo haya mafupi natumaini utaweza kukamilisha na kuficha mafaili kwa kutumia kikokotozi kwenye simu yako mkononi, lakini kumbuka kabla ya kuanza unatakiwa kuwa na simu yenye mfumo wa Android, pia hakikisha una bandle au kifurushi cha data angalau MB50 na kuendelea.

Kama unayo mahitaji hayo yote basi endelea kwa kufuata hatua hizi. Ingia kwenye soko la Play Store kisha download app inayo-itwa Calculator Vault Gallery Lock, link inapatikana hapo chini unaweza kubofya hapo na utapelekwa moja kwa moja kwenye soko la Play Store.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hiyo moja kwa moja sasa unaweza kufuata maelekezo kwenye video hpo chini ili kuweza kuset app hii.

Kwa kufuata maelekezo hayo moja kwa moja utakuwa umeweza kuficha mafile yako kwenye simu yako ya Android kwa kutumia Calculator.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video

Jinsi ya Kusajili Biashara Kupitia Google My Business (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

7 Comments