in

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12

Haya hapa mabadiliko ya muhimu yaliyopo kwenye Android 12

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12
©cnet.com

Kampuni ya Google hivi karibuni ilitangaza ujio wa mfumo mpya wa Android 12, hadi sasa yapo mambo mengi ya muhimu ambayo unapaswa kuyajua kuhusu mfumo huu mpya ambao unategemewa kuanza kutumika rasmi kwenye smartphone nyingi kuanzia mwishoni mwa mwaka 2021.

Kuliona hili leo nimeona nikuletea baadhi ya mambo ambayo utegemee kuyakuta kwenye mfumo huo mpya wa Android 12 pale simu yako itakapo pokea sasisho rasmi baadae mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2022. Basi baada ya kusema hayo twende kwenye makala hii.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Muonekano

Kwa kuanza pengine nikufahamishe kuwa mfumo mpya wa Android 12 ndio mfumo ambao unakuja na mabadiliko makubwa sana ya muonekano kuanzia mfumo wa Android Lollipop au Android 5.0. Hii ni kwa sababu Google imeleta muonekano mpya ambao umepewa jina la “Material You UI”.

Kwa haraka kabisa mabadilo ya kwanza utakayo yaona kwenye mfumo mpya wa Android 12 ni pamoja na sehemu ya Notification panel ambayo ipo juu kabisa kwenye simu yako.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12

Kwa sasa kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, sehemu ya Notification sasa inakuja na Icon kubwa na ambazo zinakuja na kona za mviringo, pia notification nazo zinakuja na muonekano wa tofauti huku nazo pia zikiwa zinakuja na kona ambazo zipo mviringo

Pia Android 12 inakuja na sehemu kubwa zaidi ya kuongeza na kupunguza mwanga wa kioo, pamoja na sehemu mpya ya Notification History ambayo utaweza kupata historia nzima ya notification zote kutoka kwenye app husika.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12

Mbali na hayo pia utaona sehemu mpya kwenye sehemu ya notification, ikiwa pamoja na sehemu mpya za settings za kamera na pia sehemu ya settings za mic.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12

Mbali na hayo pia kwenye sehemu ya lock screen kuna mabadiliko, kwani muonekano huu wa Material You UI unakuja na aina mpya za saa na widget ambazo zitakuwa na maandishi makubwa na mtindo mpya ambapo lazima utaona tofauti.

Tofauti na hayo, kwenye uwanja wa Settings pia kuna mabadiliko ya muonekano ambapo kwa sasa icon chache zimebadilishwa na kuonekana kama mfumo wa Samsung One UI. Mbali ya hayo kila sehemu kuna animation mpya pamoja na gesture ambazo unaweza kuzitumia kuendesha simu yako kwa utofauti sana.

Mabadiliko mengine makubwa ni pamoja na sehemu ya wallpaper theme, ambapo sasa ukiweka wallpaper yenye rangi, moja kwa moja rangi hiyo itaenda kuonekana mpaka kwenye Icon za simu pamoja na kurasa mbalimbali za apps na settings za simu pia zita hakisi muonekano mzima wa rangi ya wallpaper hivyo kufanya simu nzima kuwa na rangi ya wallpaper.

Materia You UI pia itaweza kufanya widget za simu yako kubadilika ikiwa pamoja na kupata rangi ambazo zitakuwa sambamba na wallpaper yako. Pia ni vizuri kukumbuka kuwa, google imeleta widget mpya kubwa ambazo zitakusaidia kufanya mambo mbalimbali ukiwa kwenye screen moja kwenye simu yako.

Kifupi ni kuwa Android 12 inakuja na mabadiliko mengi sana ya muonekano hivyo tegemea kupata muonekano mpya kwenye simu yako pale mfumo huu utakapofikia kwenye simu yako,

Ulinzi na Usalama

Kupitia mfumo mpya wa Android 12 inakuja na sehemu nyingi sana za kuboresha ulinzi na usalama. Moja ya sehemu kubwa kwenye ulinzi na usalama ni pamoja na sehemu ya “Privacy Dashboard“.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12

Sehemu hii mpya itakusaidia kuweza kujua data za muhimu kama vile ni mara ngapi app husika imetumia mic, kamera pamoja na location ndani ya masaa 24. Mbali na hayo pia utaweza kupata data nyingine za muhimu kuhusu apps mbalimbali ambazo ume install ndani ya simu yako.

Mbali na hayo, Android 12 pia inakuja na sehemu mpya ambayo itakuwa inaonyesha Mic au kamera au vyote kwa pamoja pale ambapo app fulani itakuwa inatumia vitu hivyo. Sehemu hii ni kama ile ya kwenye mfumo mpya wa iOS.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12

Pia kuitia Android 12, sasa utaweza kuchagua kama unataka kuruhusu app ijue mahali halisi ulipo, au kama unataka app ijue makadirio ya karibia na mahali ulipo. Hii itasaidia sana kwa app ambazo zina mtindo wa kutrack mtu mahali alipo, kwani sasa hazitoweza kuonyesha mahali halisi mtu alipo bali itaonyesha mahali karibu na mtu alipo endapo umewasha sehemu hiyo.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12

Mpaka sasa bado toleo la Android 12 lina endelea kuongezewa sehemu nyingi za ulinzi hivyo pengine tegemea kuona sehemu nyingi za ulinzi pale toleo hili linapofikia kwenye simu yako.

Kwa sasa hayo ndio mambo ya muhimu kwenye mfumo mpya wa Android 12 kwenye upande wa ulinzi na usalama.

Mengine ya Zaidi

Mengine ya zaidi kwenye mfumo huu mpya wa Android 12 ni pamoja na sehemu mpya ya Accessibility ambayo inakuja na sehemu mpya kama vile icon zinazoweza kukaa kujuu ya kioo chako muda wote. Hii itasaidia urahisi wa kutumia app moja na nyingine.

Sehemu nyingine ni pamoja na App hibernation ambayo huzima app ambazo hujazitumia kwa muda mrefu na kufuta data za muda mfupi ambazo huifadhiwa kwenye simu yako kupitia apps hizo.

Mbali na hayo yote Google pia inasema mfumo mpya wa Android 12 utakuwa na kasi zaidi hivyo kufanya simu nyingi kufanya kazi haraka zaidi.

Hitimisho

Kifupi ni kuwa yapo mabadiliko mengi sana kwenye mfumo wa Android 12, mabadiliko mengi bado yanaongezwa kwenye mfumo huo hivyo ni wazi kuwa utaweza kuona mengi zaidi ya haya niliyo kuandikia hapa. Kwa maoni yangu mimi binafsi, naona mfumo wa Android 12 unakuja na mabadiliko makubwa ya rangi na muonekano kuliko kitu kingine.

Kama kutakuwa na mengine usikose kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech hapa kwani ni wazi kuwa lazima tutaongelea kuhusu mfumo huu mpya wa Android 12.

Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua kuhusu mfumo wa Android 11 ikiwa pamoja na baadhi ya sifa zake. Pia kama unatumia simu ya Samsung unaweza kusoma hapa kuangalia kama simu yako ipo kwenye simu zitakazo pokea mfumo wa Android 12 hivi karibuni.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 12
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments