Jinsi ya Kurekodi Video za Time-Lapse Kupitia Simu (Android)

Apps ambazo zinaweza kukusaidia kurekodi video za Time-lapse kwa urahisi
Jinsi ya Kurekodi Video za Time-Lapse Kupitia Simu (Android) Jinsi ya Kurekodi Video za Time-Lapse Kupitia Simu (Android)

Kama wewe ni mpenzi wa kurekodi video mbalimbali au unajifunza photography au videography basi ni wazi unajua kuhusu video za Time-Lapse, kama kwa namna yoyote hujui maana ya Time-Lapse hizi ni picha ambazo huchukuliwa kwa vipande tofauti na baadae kuunganishwa na kutengeneza video.

Ili uweze kuweze kuelewa kuwa urahisi angalia video hapo chini kuweza kuona mfano wa video ya Time-lapse.

Advertisement

Kama unavyoweza kuona video hiyo ni Time-Lapse ya haragwe likiwa linaota kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya mwisho. Unaweza kurekodi video hizi moja kwa moja kwa kitumia simu yako ya mkononi kwa kutumia apps zifuatazo.

Framelapse ni moja kati ya apps bora sana ambayo inaweza kusaidia sana kutengeneza Time-lapse, app hii ni moja kati ya app bora sana na inakupa uwezo wa kubadilisha vitu mbalimbali kama vile kuweka filters mbalimbali kwa urahisi na haraka. Mbali na hayo app hii ni rahisi sana kutumia.

Download App Hapa

Lapse It ni app nyingine ambayo inakupa uwezo wa kurekodi Time-lapse kwa urahisi na haraka, app hii pia ni rahisi sana kutumia na ukweli haitaji maelezo kwa muda mrefu. Unaweza kuangalia video hapo chini kuelewa kidogo jinsi ya kurekodi video za Time-lapse kupitia app ya lapse it.

Download App Hapa

App nyingine ambayo inaweza kusaidia kurekodi video za Time-Lapse ni pamoja na app ya Microsoft Hyperlapse Mobile, app hii pia inaweza kurekodi video za Time-lapse kwa speed mbalimbali na unaweza kubadilisha kila kitu kupitia app hii ambayo imetengenezwa na kampuni ya Microsoft. Mbali ya yote pia utaweza kushare video zako kwenye mitandao ya kijamii.

Download App Hapa

Time Lapse camera
Price: Free

App nyingine ya Android ambayo unaweza kutumia kurekodi video za Time-lapse ni pamoja na app ya Time Lapse camera. App hii ni bora na rahisi kutumia na unaweza kurekodi video kulingana na speed utakayo chagua ndani ya app hii. Unaweza kupakua app hii kupitia hapo chini.

Download App Hapa

App nyingine kwenye list hii ni pamoja na app ya PicPac Stop Motion & TimeLapse
, app hii haina tofauti na app nyingine hapo juu tofauti kubwa iliyopo kwenye app hii ni kuwa unaweza kuendesha app hii kwa kutumia sauti yaani voice command. Download app hii hapo chini kujua zaidi sehemu zote za app hii.

Download App Hapa

Na hizo ndio apps ambazo zinaweza kusaidia kuweza kurekodi video za Time-Lapse kwa urahisi na haraka. Kama unataka kujifunza zaidi jinsi ya kurekodi video bora kwa kutumia simu yako ya mkononi basi unaweza kusoma makala yetu hapa.

Kama unataka kuendelea kujifunza zaidi vitu mbalimbali vya teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use