in

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Simu nyingine kutoka Infinix yenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Katika ulimwengu wa kisasa simu janja ni chombo muhimu sana katika pirikapirika za kila siku lakini ni vipi unaweza timiza malengo yako ya siku pasipo kuwa na Infinix HOT 10 play yenye battery yenye ujazo wa mAh 6000.

Kampuni ya simu Infinix ilitangaza Infinix Hot 10 na Hot 10 Lite mwaka jana, na mnamo wiki ya jana kampuni hiyo imeongeza simu mpya katika toleo hilo la HOT 10 yenye kufahamika kama HOT 10 play.

Akizungumza na waandishi wa habari kutoka kwenye ofisi zetu, Afisa Mahusiano Aisha Karupa alisema, “Infinix HOT 10 play tumeitambulisha rasmi kupitia mtandao wa kijamii @infinixmobiletz 28/1/2021, ni simu ya kila mtu, ni simu rafiki kwa wenye kipato cha kati na cha chini pia na ni rafiki kwa anaefikiria kuingia katika ulimwengu wa simu janja, basi Infinix HOT 10 play ni simu sahihi kwake.

Infinix HOT 10 play inapatikana katika maduka yote ya simu ikiwa na sifa zifuatazo kama vile mAh 6000 za battery zenye kukuhakikishia matumizi ya simu yako kwa siku nzima na zaidi”.

Shina Zawadi Kibao Kupitia TECNO Spark 9 na CAMON 19

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Infinix Hot 10 play inaendeshwa na processor ya Helio G25 SoC na Android 10 (Toleo la Go) XOS 7.1.Muonekano wa mbele wa Infinix HOT 10 play umetawaliwa na wigo mpana wa kioo chenye inchi 6.82 HD na MP 8 za kamera. Muonekano wa nyuma wa Infinix HOT 10 play ni wakupendeza ulionakshiwa na MP 13 za  kamera mbili pamoja na fingerprint.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Uwezo wa kuhifadhi vitu/kumbukumbu/memory ni mkubwa. HOT 10 play inaujazo wa GB2/GB32 na GB4/64GB zenye nafasi kubwa kwa uhifadhiaji kumbukumbu nyingi sana kama vile picha, video, miziki na kadhalika” alimalizia.

Tembelea katika maduka yote ya simu ili kujipatia Infinix HOT 10 play sasa kutoka Infinix, vile vile usiache kutembelea tovuti ya infinix kujua zaidi.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment