in

Tetesi : Instagram Kuja na Sehemu ya Link Kwenye Description

Instagram kuanza kuruhusiwa kuweka link kwenye description kwa pesa

Tetesi : Instagram Kuja na Sehemu ya Link Kwenye Description

Kwa muda mrefu watumiaji wa mtandao wa Instagram wamekuwa wakitamani kupata sehemu ya kuweka link kwenye description ya picha na video mbalimbali kupitia mtandao wa Instagram, hivi karibuni inasemekana kuwa instagram wanaweza kuwezesha sehemu hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Verge, instagram imebainika kufanya mpango wa kuleta sehemu ya kuweka link kwenye description, sehemu ambayo inasemekana kuwa itakuwa inalipiwa ili uwezesha link kupitia sehemu hiyo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Tetesi : Instagram Kuja na Sehemu ya Link Kwenye Description

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, Instagram imeonyesha jinsi sehemu hiyo itakavyofanya kazi. Kupitia mchoro huo, instagram imebainisha kuwa pale mtumiaji atakapo weka link kwenye sehemu ya maelezo kupitia picha au video, moja kwa moja ataletewa maelezo ambayo yata muhitaji kulipia ili kufanya link hiyo kuweza kubonyezeka.

Kama unavyojua sehemu ya maelezo au description kwenye mtandao wa instagram haina uwezo wa kufanya link iweze kubonyezeka na hivyo link yoyote ambayo itawekwa kwenye sehemu hiyo huwa kama maandishi ya kawaida tu.

Kwa sasa hakuna taarifa zaidi za lini sehemu hii inaweza kuwezeshwa kwa watumiaji mbalimbali kote duniani, huku pia kukiwa na tetesi kuwa sehemu hii inaweza isije kabisa kwa watumiaji wote kutoana na kuwa zipo sehemu nyingi ambazo zilikuwa kwenye hatua ya ubunifu lakini hadi leo hazijafanikiwa kutoka kwa watumiaji mbalimbali wa mtandao huo.

UPDATE 14-09-2020 : Baada ya taarifa hizi kwenda hewani, Instagram kupitia mtandao wa The Verge imetangaza kuwa haina mpango wa kuweka link kwenye sehemu ya description.

Kwa sasa njia pekee ambayo unaweza kutumia kuweza kuweka link kwenye akaunti yako ya Instagram ni kuweka link kwenye sehemu ya Bio. Kama unataka kuweka link zaidi ya moja kupitia sehemu ya bio basi unaweza kusoma hapa kujua mitandao ya kukusaidia kufanya hivyo.

Google Kuzindua Simu Mpya za Pixel 8 Mwezi Oktoba (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.